KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA VICTOIRE INGABIRE AHUKUMIWA MIAKA 8 JELA.
Posted on
Oct 30, 2012
|
No Comments
Kiongozi
wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire (pichani) amepatikana na
hati katika kesi ya uhaini iliyokuwa ikimkabili na kuhukumiwa adhabu ya
kifungo cha miaka nane jela.
Upande wa mashitaka ulitaka ahukumiwe kifungo cha maisha kwa makosa aliyokuwa akishitakiwa nayo ya kutishia usalama wan chi.
Mahakama pia imemuona kuwa na hatia ya kudharau mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
Hata
hivyo Ingabire hakuwepo mahakamani kusikiliza hukumu dhidi yake kwa
kuwa aliigomea kesi hiyo akisema inachochewa na masuala ya kisiasa.