LIL WAYNE ALAZWA HOSPITALINI, SABABU ZIKISEMEKANA NA "DRUG OVERDOSE"
Posted on
Oct 27, 2012
|
No Comments
Rapper mkali toka YMCMB Lil Wayne ameripotiwa kulazwa
hospitalini mara mbili ndani ya saa 24 kwa kile ambacho kinaelezwa kuwa ni
‘seizure’, iliyompata kwa mara ya pili akiwa ndani ya private jet akitokea
Texas kwenda LAX...
Mtandao wa TMZ uliambiwa na mtu wa karibu wa Weezy kuwa ndege
hiyo ilikatiza safari yake na kuelekea Louisiana baada ya hali ya mkali huyo wa
michano kubadilika ambapo alipelekwa hospitalini haraka kwa matibabu.
Hata hivyo taarifa za awali toka hospitalini hapo zilionesha
kuwa Lil Wayne anaendelea vizuri na muda wowote angeweza kutolewa hospitalini
hapo.
Tofauti na ugonjwa ambao watu walikuwa wanajua ndio
unaomsumbua Weezy, Management yake ilitoa tamko kuhusu kile kinachomsibu rapper
huyo baada ya taarifa za ku-seize hapo jana kwa mara ya kwanza.
“Lil Wayne aliweza kutolewa hospitalini baada ya matibabu kwa
ajili ya maumivu makali ya kichwa na vilevile upungufu wa maji. Yuko
nyumbani amepumzika chini ya uangalizi
wa daktari na atarudi kazini hivi karibuni. Ana-appreciate fans wake kwa sapoti
yao na anawapenda.” Hilo ndilo tamko la management yake.
Ripoti zinazohusu hali ya Weezy kulazwa kwa mara ya pili
hospitalini kwa ugonjwa wa ‘seizure’zilisambaa katika mitandao mbalimbali na
watu wakatoa maoni tofauti tofauti kuhusu hili kwa sababu ugonjwa huu
unaconnection kubwa sana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Wengine waliuliza ‘could it have been a drug overdose??”
lakini taarifa za kitaani tu zinasema alikuwa anakunywa sana siku hiyo na kuwa
wanaunganisha ugonjwa huo na matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya.
Mshindi huyo wa tuzo za Grammy aliruhusiwa kutoka hospitalini
hapo kama taarifa za management yake zilivyosema.
Matumizi ya madawa ya kulevya yamekuwa yakiwatesa sana mastaa
nchini Marekani, hali hii ndiyo
inawafanya watu waunganishe hali ya afya ya Lil F.Baby na kutumia madawa
ya kulevya kupita kiasi ‘drug over dose’.