MAJINA YA WALIOHUSIKA KUMUUA KAMANDA BARLOW MWANZA YAMETAJWA, NDIO HAYA.
Posted on
Oct 26, 2012
|
No Comments
Mwandishi wa habari Albert G Sengo kutoka Mwanza ameripoti kwamba majina ya watu watano wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Leberatus Barlow yametajwa na Polisi.
Akitaja hayo majina mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jinai
(DCI), Robert Manumba amesema simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye
alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha
upelelezi huo na wahusika kukamatwa.
Waliotajwa kuhusika na
hayo mauaji ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye ametajwa kwamba ndiye
aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48),
Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote
wamekatwa wakiwa Dar es Saalam walipokimbilia baada ya mauaji.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa Dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine Lakini chanzo cha hao wauaji kufanya hivyo bado hakijatajwa.
Liberatus Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi
mitatu huko Kitangiri wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy
Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa
wa Rufiji.