MTETEZI WA WANAWAKE ANUSURIKA KIFO DRC
Posted on
Oct 26, 2012
|
No Comments
Mtetezi maarufu wa wathiriwa wengi wa ubakaji katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo amenusurika jaribio la kumuua.
Daktari Denis Mukwege alishambuliwa na watu
waliokuwa na bunduki nyumbani kwake Bukavu aliko na hospitali
inayowahudumia waathiriwa wa dhulma za kimapenzi.
Alihepa risasi lakini mlinzi wake aliuawa katika tukio hilo.
Daktari Mukwege ni mpasuaji mashuhuri duniani na
ameshinda tuzo nyingi tu kimataifa kwa juhudi zake kutetea wanawake
wanaobakwa na makundi ya waasi.