UCHUMI WA DUNIA WATETEREKA ZAIDI
Posted on
Oct 9, 2012
|
No Comments
Shirika la fedha duniani IMF linasema kuwa kumekuwa na vikwazo vipya katika kujaribu kuunusuru uchumi wa dunia .
Shirika hilo linasema kuwa halina matumaini
makubwa kuhusu kuchepuka kwa uchumi wa dunia na linatarajia uchumi wa
kanda ya Euro kuanguka zaidi kwa asilimia nusu mwaka huu.
Katika ripoti yake mpya shirika la IMF linasema
tatizo kubwa ni kwamba sera za uchumi katika nchi zilizoendelea
zimeshindwa kujenga upya imani ya ukuwaji wa uchumi .
IMF sasa imeshusha viwango vyake vya matarajio
ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa kiwango cha asilimia tatu kwa mwaka huu
na mwaka ujao na kusema kuwa matumaini ya ukuwaji yatakuwa juu mwaka
ujao.
Limesema kuwa sera katika nchi zilizostawi, zimekosa kujenga matumaini na hivyo kusababisha hali ya taharuki katika masoko ya Ulaya.