photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > UHABA WA MAJI WACHANGIA KUDUMAZA KIWANGO CHA ELIMU SEKONDARI YA MALULA WILAYANI ARUMERU.

UHABA WA MAJI WACHANGIA KUDUMAZA KIWANGO CHA ELIMU SEKONDARI YA MALULA WILAYANI ARUMERU.

Posted on Oct 8, 2012 | No Comments

Uongozi wa shule ya sekondari ya Malula iliyopo King”ori wilayani Arumeru Mashariki mkoani Arusha umeiangukia serikali na kuiomba itatue tatizo la kero ya maji inayowakabili shuleni hapo kwa madai kwamba linachangia kudumaza kiwango cha elimu shuleni hapo.
Hatahivyo, uongozi huo umesisitiza ya kwamba wanafunzi wa shule hiyo wanalazimika kutembea umbali mrefu kusaka huduma hiyo na kujikuta wakipoteza muda mwingi wa masomo.
Akizungumza katika mahafali ya kwanza shuleni hapo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mkuu wa shule hiyo Rehema Mroso amesema kwamba shule yake imekuwa ikikabiliwa na tatizo kuu la uhaba wa maji tangu ianzishwe huku akiiomba serikali iwajengee matanki ya kuhifadhi maji kuokoa tatizo hilo.
Mroso amesema kwamba baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kolomita 5 kusaka maji kitendo ambacho kimechangia kudumaza kiwango chao cha elimu kwa kuwa wanatumia muda mwingi kusaka maji.
Amesema kwamba tatizo la uhaba wa maji limechangia kuharibu mazingira shuleni hapo kwa kuwa hukosa maji ya kuboreshea mazingira sanjari na kusafishia vyoo mbalimbali shuleni hapo.
Hatahivyo amesisitiza kwamba wamekuwa wakikabiliwa na kero za uhaba wa jengo la utawala, maabara, uhaba wa nyumba za walimu sanjari na tatizo la uzio wa shule hali ambayo inahatarisha usalama wa wanafunzi hususani wa kike wanaolala shuleni hapo.
Awali akizungumza katika mahafali hayo mgeni ramsi ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Exauds Mwanga, amesema kwamba serikali imepokea  na italifanyia kazi tatizo la kero ya maji lakini amewashauri kupanda miti ya kutosha kwa lengo la kuhifadhi  mazingira shuleni hapo.
Aidha Mwanga ameikemea tabia ya baadhi ya wanafunzi hususani wa kiume shuleni hapo kuvaa suruali zao chini ya makalio maarufu kama  “mlegezo” huku akisisitiza ya kwamba uvaaji huo ni marufuku hapa nchini.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru