photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > UPUNGUFU WA MAFUTA TANZANIA UBABE WA EWURA NA TRA

UPUNGUFU WA MAFUTA TANZANIA UBABE WA EWURA NA TRA

Posted on Oct 30, 2012 | No Comments


Kumekuwa na upungufu mkubwa wa mafuta ya Petrol, Diesel na mafuta ya Taa.

Na hii imesemekana ni kutokana na EWURA kupunguza bei ya mafuta siku chache zilizopita.

Serikali kwa kupitia EWURA wameamua sas kusitisha usafirishaji wa mafuta nchhi za nje (TRANSIT GGODS) ili yatumike hapa nchini, kitu ambacho kinaleta utata kwani hayo mafuta ya TRANSIT siyo mali ya Serikali bali yanapaswa kupelekwa nchi husika. Lakini Serikali wanatumia ubabe katika suala hili badala ya kutafuta mbinu nzuri ya kuondoa upungufu wa mafuta nchini.

Ubabe kama huu hausaidii kwani inaweza kusababisha nchi za Zambia, Rwanda, Congo, Burundi ambao wanapitisha mafuta hapa Bandari zetu wakaamua kuhama Bandari za nchi mfano Mombasa au Beira kitu ambacho kitainyima mapato TRA kwa kiasi kikubwa.

Ni wakati kwa Serikali yetu kutafuta mbinu mpya au waifufue TIPER ili wasafishe mafuta na kupunguza hali kama hii ya upungufu isitokee.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru