UVCCM WAPEANA KIPIGO LAIVU KWENYE UCHAGUZI, ANGALIA >>
Posted on
Oct 9, 2012
|
No Comments
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana wa
CCM, UVCCM mkoani Mara, ulikumbwa na songombingo nguo kuchanika baada ya
vijana hao kuzua ugomvi na kupeana kichapo cha nguvu. Kwenye vurugu
hizo, licha ya kutwangana ngumi, wadau hao walirushiana viti, mawe na
silaha mbalimbali za jadi ndani na nje ya ukumbi wa mkutano jambo ambalo
lilisababisha mkutano huo kuvunjika.