WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ITALIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 4 JELA.
Posted on
Oct 28, 2012
|
No Comments
Silvio Berlusconi.
Mahakama
moja mjini Milan imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio
Berlusconi kifungo cha miaka minne gerezani kwa kukwepa kulipa kodi na
kumpiga marufuku kushikilia wadhifa wa umma kwa miaka mitatu.
Uamuzi
huo wa mahakama umekuja siku mbili baada ya mfanyabiashara huyo na
mwanasiasa mwenye umri wa miaka 76, kutangaza kuwa hatagombea tena
nafasi ya Waziri Mkuu katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Mwendesha
mashitaka Fabio De Pasquale amehoji kuwa kampuni ya habari ya
Berlusconi, Mediaset, ilikuwa na mfumo wa kifedha wa kuongeza kiholela
malipo ya haki miliki za televisheni kutoka Marekani kwa njia ya kampuni
zilizosajili nje ya nchi.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka kampuni ya Berlusconi ilikwepa Klipaji kodi yenye thamani ya Euro bilioni 14 kwa miaka kadhaa.