DIWANI MATATANI KWA FEDHA ZA UJENZI WA SHULE
Posted on
Nov 12, 2012
|
No Comments
WANANCHI wa Kata ya Bwera, wilayani Chato,
mkoani Geita wamemlalamikia diwani wao, Elam Lubagola wakidai katumia
vibaya Sh4 milioni fedha za ruzuku ya maendelo kwa ajili ya ujenzi wa
shule ya sekondari ya kata, zilizotolewa na halmashauri ya wilaya mwaka
2006.
Baadhi ya wenyeviti wa vitongoji na vijiji pamoja na watendaji wa vijiji vya Busaka, Bwera na Igando wamesusia kuwasomea wananchi taarifa za mapato na matumizi hususa michango ya ujenzi wa shule hiyo ili kumshinikiza diwani atoe maelezo.
Kufuatia hali hiyo wananchi wa kata hiyo wamelalamikia diwani wao kwa ukimya na kumtaka atoe maelezo hayo.
Diwani Lubagola alipoulizwa alisema fedha zote zilitumika kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mkuu wa Shule na jengo la utawala pamoja na kuwalipa wakandarasi waliohusika katika ujenzi huo wa shule.
Hata hivyo kauli hiyo ilipingwa vikali na Mwenyekiti wa Kijiji cha Busaka, Faustine Sosoka.
Pamoja na diwani huyo kukanusha kuhusika kutafuna fedha hizo, mwenyekiti huyo alisema wakandarasi wa ujenzi wa shule hiyo tangu mwaka 2007 hawajalipwa fedha zao na baadhi yao wamekata tamaa ya kuzidai.
''Diwani wa kata yetu anarudisha nyuma maendeleo yetu,tumechanga Sh18,000 kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa shule yetu, lakini sasa tukiwahojiwa wenyeviti wetu kutusomea taarifa za mapato na matumizi,wanadai mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata WODC, diwani hataki, hadi sasa hatujui hatma ya fedha zetu''alisema Joseph Lugembe.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato,Shabani Ntarambe alipotakiwa kuzungumzia sakata hilo, alisema yeye siye msemaji wa halmashauri na kudai kwamba msemaji ni mkuu wa wilaya ambaye naye Rodrick Mpogolo alipoulizwa kuhusiana na tuhuma za diwani huyo alisema hana taarifa na kuahidi kulitolea ufafanuzi suala hilo mwishoni mwa mwezi huu.