photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > DKT. MWAKYEMBE AFUTA BODI YA WAKURUGENZI WA BANDARI (TPA) NA KUTEUA WAPYA.

DKT. MWAKYEMBE AFUTA BODI YA WAKURUGENZI WA BANDARI (TPA) NA KUTEUA WAPYA.

Posted on Nov 8, 2012 | No Comments

Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) (pichani) amefuta uteuzi wa Wajumbe wote wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (TPA) na kuteua Wajumbe wapya wanane wanaounda Bodi hiyo.
Waziri amechukua uamuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya Bandari na Kifungu cha 1(2)(i) cha Jwdwali la Kwanza la Sheria ya Bandari ya 2004.
Mabadiliko hayo ni sehemu tu ya hatua ambazo Wizara inachukua kurejesha ufanisi katika Mamlaka hiyo ili iweze kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa.
Aidha Waziri ameiagiza Menejimenti ya TPA kuwapa nyaraka zote muhimu Wajumbe wa Bodi ili wajiandae kabla hajakutana nao ndani ya simu 10 ili kuingia nao Mkataba wa Ufanisi (Performance Contract).
Waliofutiwa Ujumbe wa Bodi ni:
1. Bw. Dunstan G. Mrutu.
2. Eng. George H. Ally.
3. Mh. Alh. Mtutura A. Mtutura (Mb).
4. Bw. Emmanuel Mallya.
5. Bibi Mwanmtumu J. Malale.
6. Bibi Maria N. Kejo.
Kwa bahati mbaya wajumbe wawili wa Bodi hii walipoteza uhai hivi karibuni.
Walioteuliwa kuingia kwenye Bodi hiyo ni:
1. Dkt. Jabiri Kuwe Bakari.
2.Bw. John Ulanga.
3. Bi. Caroline Temu.
4. Bw. Jaffer Machano.
5. Dkt. Hildebrand Shayo.
6. Bw. Saidi Salum Sauko.
7. Eng. Julius Mamiro.
8. Bi. Asha Nassoro.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru