KAULI YA DAVID KAFULILA KUHUSU MKUU WA MKOA WA KIGOMA.
Posted on
Nov 30, 2012
|
No Comments
David Kafulila.
Mbunge wa jimbo la Kigoma
kusini DAVID KAFULILA amesema anakusudia kupeleka hoja binafsi kwenye
kamati ya maadili ili iweze kumchukulia hatua mkuu wa mkoa wa Kigoma
luteni kanali mstaafu ISSA MACHIBYA kwa madai ya kulidhalilisha Bunge
ambalo ni muhimili wa serikali.
Akiwa kwenye kongamano la
kujadili masuala ya uwekezaji katika kanda ya ziwa Tanganyika
lililofanyika mkoani Katavi hivi karibuni, mkuu huyo wa mkoa wa Kigoma
anadaiwa kutoa kauli kuwa wabunge ambao hawatafuata maelekezo yake kama
mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya watapigwa pingu kama raia wa kawaida.
Kanali mstaafu Issa Machibya.
Kauli hiyo imeonekana kuwakwaza
wabunge wa mkoa wa Kigoma ambao wamesema huko ni kukiuka sheria na
kuudhalilisha mhimili wa Serikali na hivyo mbunge huyo wa Kigoma kusini
amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuomba radhi vinginevyo atamshitaki.
Mbunge Kafulila Amesema anashangaa ni kwa nini spika wa bunge bi.Anne Makinda amekaa kimya bila kusema lolote juu ya