MAWAKILI WA VIONGOZI WA UAMSHO WALALAMIKIA HALI YA WATEJA WAO GEREZANI.
Posted on
Nov 8, 2012
|
No Comments
Mawakili
wa Viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar
(JUMIKI ) wamesema kuwa wateja wao waliokamatwa siku 17 zilizopita kwa
tuhuma za kuchochea vurugu kisiwani Unguja, hawatendewi haki na wanapata mateso makubwa gerezani wanakoshikiliwa ikiwemo kunyolewa ndevu.
Mawakili
hao wakiongozwa na Salim Tawfiq wanasema kwa sasa wateja wao hawapaswi
kutendewa visa kama hivyo kwa kuwa bado ni watuhumiwa na kwamba
hawajatiwa hatiani.