photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > MAMILIONI YALIWA KINYEMELA HOSPITALI YA RUFAA

MAMILIONI YALIWA KINYEMELA HOSPITALI YA RUFAA

Posted on Nov 12, 2012 | No Comments


Mganga mfawidhi (medical officer in charge) wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, BOMBO dr. Karia, kaimu wake dr.Naima ,muhasibu wa hospitali na kiongozi wa interns wa hospitali ya BOMBO dr. Mwema wameshirikiana kuiba pesa za walipa kodi tsh 8,861,000 (milioni nane na laki nane) kupitia malipo hewa ya madaktari mafunzoni (intern doctors) 10 (kumi) ambao wameshamaliza internship na kuondoka ya October 2012 kutoka wizara ya afya.
Mwaka 2011/2012 hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga,bombo ilikuwa na intern doctors 31 na intern mmoja wa maabara ambao walianza intern yao kadili walivyofika kuanzia 03/october/2012. september 2012 interns 32 waliombewa posho zao za kujikimu za mwezi september. kati ya hao 32 interns doctors 10 yalikuwa ni malipo stahiki yao ya mwisho kwani walimaliza trh 02/october na hivyo hawakustahili posho ya kujikimu ya october 2012. na wote waliondoka wakijua kwamba hawaidai wizara ya afya kwani wamefanya intern kwa miezi 12 na wamelipwa posho miezi 12, wakapewa vyeti vyao na wakaondoka.
Ila jambo la kushangaza mganga mfawidhi wa hospitali dr. karia , kaimu wake wake dr naima,kiongozi wa intern dr. mwema na muhasibu wa hospitali waliwaombea kinyemela hao interns doctors 10 malipo hewa ya mwezi october 2012 wakijua fika hawastahili na ni kufisadi kodi za wananchi.
Wizara ya afya ilituma malipo ya posho ya kujikimu ya October/2012 kwa interns wa bombo ikiwa na ziada ya malipo hewa ya tsh 8,816,000 (milioni nane na laki nane) kwa interns doctors ambao wameshamaliza intern na kuondoka tanga. trh 07/november/2012 muhasibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa tanga, bombo alianza kugawa posho ya kujikimu kwa interns waliokuwa wanaendelea na wale wapya. na wale interns waliokuwa wanaendelea(walioanza 2011 kwa kuchelewa) walishangaa kuona majina ya wenzao waliomaliza muda wao na kuondoka yapo kwenye karatasi ya kusaini wakati wa kulipwa huku wakiwa wameghushiwa sahihi mbele ya majina yao kwamba wamechukua pesa wakati hawapo kabisa tanga na wala hawana taarifa kwamba watalipwa posho ya october/2012.
Doctors 10 walioombewa malipo hewa ni: dr. Abasi, dr. Rajab Hussein, dr. Hussein Sepoko, dr. Awe, dr.Gladys Yona, dr. Serina, dr.Patrick, dr. Zaharia, dr. Agnes, na dr. Daniel. Baadhi ya hao walioombewa malipo hewa wakiwemo tayari wameshapata usajili wa muda wa baraza la madaktari tanganyika(mct temporary registration).
Tayari maombi posho ya kujikimu kwa interns wa hospitali ya rufaa ya mkoa tanga, bombo ya november/2012 yamekisha wasilishwa wizara ya afya na kiongozi wa interns wa bombo dr. mwema, hatujui hayo maombi yatakuwa na malipo hewa ya kiasi gani.
kweli nchi hii inaliwa sana, na hii ni hospitali moja yenye interns, inawezekana hospitali zingine zinafanya mchezo huu hivyo wizara ya afya inapoteza mamilioni mengi kwa malipo hewa.
nawasilisha wanajamvi.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru