MWANAMITINDO ALBINO JE INAWEZEKANA?.
Posted on
Nov 2, 2012
|
No Comments
Diandra Forrets akijiandaa kwa maonyesho ya mitindo nchini Afrika Kusini
Nyuma ya
ukumbi, kelele zikiwa zimejaa katika tamasha la Wiki ya mitindo Afrika
nchini Afrika Kusini, mwanamke mmoja amekaa kimya.
Wanamitindo wenzake pamoja na wabunifu wa
mitindo kutoka kote barani Afrika wana kazi nyingi si haba. Kuna
shughuli si haba kiasi cha mtu kusema kuwa kuna ushindani wa kelele.
Lakini licha ya kimya chake, Diandra Forrest mwanamitindo wa kulipwa raia wa Marekani, ndiye nyota ya chumba hiki.
“Ni muhimu kwangu kuwa hapa kwa sababu nataka
kubadili ambavyo watu wanavyowatizama wasichana maalbino katika bara
hili.” Alisema Diandra
Akiwa na ukosefu wa rangi katika ngozi yake au
nywele zake, msichana huyo aliyekulia mjini New York, hususan katika
mtaa wa Bronx ambao ni makao kwa wamarekani weusi, ni kawaida kwake kuwa
na tabasamu.
Takriban mtu mmoja kwa kila watu 17,000
anazaliwa akiwa na hitifalu katika genetiki zake ambayo inaweza
kumsababisha kuwa kipofu au kuwa na ulemavu wa ngozi.
Lakini anajua kuwa kuwepo kwake hapa katika
maonyesho ya mitindo ya kiafrika, ina umuhimu mkubwa kuliko kuhoji dhana
ya ''ni nini urembo?''
Katika baadhi ya nchi za afrika, hasa Afrika
Mashariki, watu anbao ni Albino, wanaishi katika hofu ya kutekwa na
kuchinjwa kwa sababu viungo vya miili yao vinaaminika kuwa na nguvu
fulani.
"Ni muhimu kwangu sana kuwa hapa kwa sababu
nataka kubadili dhana za watu kuhusu wasichana walio na ulemavu wa
ngozi’’ aliambia BBC
"Nilidhani kuwa maisha yalikuwa magumu kwangu
nilipokuwa mtoto, watoto wengine wakinikejeli saa zote. Kila nikienda
nyumbani nilikuwa nalia’’ alisimulia Diandra.
'Apigwa na butwaa'
" Lakini hiyo sio hoja ikilinganishwa na kile
ambacho watu kama mimi hupitia katika safu kama hii, hususan katika
maeneo ya mashinani’’
Watengezaji wa mtindo, wa kimataifa wanawatumia maalbino sana siku hizi katika kuonyesha mitindo yao.
“Nilipogundua kuwa katika nchi kama Tanzania,
maalbino kama mimi wanaishi na hofu ya kukatwa sehemu zao za mwili kwa
sababu za kibiashara, nilipigwa na butwaa. Watu kama mimi wanaishi kwa
hofu kila siku ya maisha yao. Inasikitisha sana.’’
Lakini inapokuja kwa mitindo ya kimataifa Bi Forrest anatoa mwelekeo.
Kama wengine, katika sanaa ya mitindo, msanii wa
Afrika Kusini anayeishi uingereza, Jacob Kimmie alifurahi sana
alipokutana na Bi forrest.
"Anaonekana tofauti sana na ana mvuto ambao
sijawahi kuona kama mwanamitindo. Niliona kama lazima kuwa naye mwenye
tamasha la leo.’’ Alisema Jacob.
Wakati huu katika safu za mitindo, kumtumia
mwanamitindo Albino katika maonyesho yoyote , ni kitu kinachowika sana
sasa. lakini natumai kuwa kutumia watu kama hawa kutaleta mabadiliko
yatakayodumu’’
Refilwe Modiselle, mwanamitindo wa Afrika Kusini, na ambaye ni Albino aliyekulia mtaani Soweto,anakubaliana na kauli hii.
Kazi yake ya uwanamitindo ilianza tangu akiwa na
umri wa miaka 13, na sasa yeye ndiye sura ya kampuni ya mitindo ya
Legit na anasema kuwa wakati huo mtu yeyote aliyekuwa albino alibaguliwa
sana.
"Nahisi kuwa kazi ambayo Diandra na mimi tunafanya ni kuleta mabadiliko ya kweli.’’ Anasema Modisile
Ushirikina
Lakini katika mkoa wa Kwazulu Natal, siku moja
baada ya kuanza kwa tamasha hili, inaarifiwa mtoto mmoja mvulana
hajulikani aliko mwaka mmoja baada ya kutekwa nyara.
Maalbino wamekuwa waathiriwa wa mauaji ya kishirikina
Familia yake inahofia kuwa huenda alitekwa kwa sababu za kishirikina
Na hivi karibuni, katika eneo la Meru, nchini
Tanzania maiti ya mwanaume anayeonekana alikuwa na umri wa miaka 30,
ilipatikana mwezi Juni ikiwa haina baadhi ya sehemu za mwili wake.
Sasa je sanaa ya mitindo inaweza kuleta mabadiliko?
Peter Ash, mwandishi wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu masaibu ya maalbino, anasema inawezekana
“Kadri ujumbe kama huu unavyoendelea kutolewa
kuhusu maalbino, ndivyo mambo yanakvokuwa sawa juu yao. Kwa hakika
itasaidia” alisema Ash
"Tunavyoona ni kwamba dhulma dhidi ya albino ni
kama zinakubalika katika jami kwa sababu wanaonekana kama sio watu kama
wengine. Wanaonekana kama laana au wanawakilisha ushirikina’’ anasema
Ash.
Kwa hivyo ni muhimu kwa jamii za kiafrika kuanza kuona watu kama hawa ambao wanaleta mabadiliko katika dhana kuhusu maalbino’’
“Mimi ni msichana mweusi mwenye ngozi ya mtu
mweupe na hilo pekee linapaswa kuleta taswira ya binadamu na anachopaswa
kuwakilisha
Katika ripoti ya umoja wa mataifa iliyofanywa na
Ash,takriban watu 71 waliuawa nchini Tanzania kati ya mwaka 2006 na
2012, na wengine 31 wakanusurika mauaji.
Maalbino kumi na saba waliuawa nchini Burundi, saba nchini Kenya na wengine watatu nchini Swaziland.
Visa vya mauaji havikutokea sana nchini Afrika
Kusini anasema Nomasonto Mazibuko kutoka kwa shirika linalotetea maslahi
ya wenye ulemavu wa ngozi
Lakini anasema kuwa mabadiliko yanapaswa kuja kutoka ndani ya bara la Afrika.
“Swala nyeti hapa ni watu hawaoni maalbino kama binadamu. Ni juu yetu kuzungumzia swala hili na kuweza kuangamiza unyanyapaa.”
Anaongea kwa ukali “Hatuwezi kukimya wala
hatuwezi kujificha. Na msichan yeyote ambaye ni albino na ambaye yuko
katika jukwaa la kimataifa la mitindo au hata kwenye barabara akiwa
anajivunia, ni kiungo kinachohijitajika kuweza kuwa moyo wasichana
wengine’’
Bi Modiselle anatumai kuwa yeye atakuwa chachu ya mabadiliko
"mimi ni ishara ya umoja. Mini ni msichana mweusi mwenye ngozi nyeupe
" Ningependa kusifika tu kama mwanamitindo wala sio kwa sababu ya ulemavu wangu wa ngozi.’’ aliongeza Modisile