MWANAMKE WA KWANZA WAZIRI WA SOMALIA
Posted on
Nov 4, 2012
|
No Comments
Waziri mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon ndiye ameteua baraza hilo la mawaziri
Somalia inatarajiwa kupata
waziri wake wa kwanza mwanamke pinde baraza la mawaziri
lililopendekezwa na waziri mkuu Abdi Farah Shirdon litakapoidhinishwa na bunge.
Fauzia Yusuf Haji Adan ni mmoja wa wanasiasa
kumi waliteuliwa katika baraza la mawaziri ambalo ni ndogo sana na
ameteuliwa kama waziri wa mambo ya nje.
Alitaja kuteuliwa kwake kama jambo
la kihistoria kwa nchi hiyo na kwa wanawake wa Somalia. Bi Fauzia pia ni
naibu waziri mkuu wa Somalia.
Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa bwana Shirdon huenda akakabiliwa na kibarua kutafuta kupitishwa kwa baraza hilo na kuna hofu kuwa koo zote huenda zisiwakilishwe kikamilifu.
Bwana Shirdon, ambaye ni mfanyabiashara alichukua wadhifa wake baada ya kuteuliwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud na hata kukubaliwa na bunge.
Uchaguzi wa bwana Mohamud mwezi Sepetemba alionekana kuwa Rais wa kwanza wa Somalia kuchaguliwa kidemokrasa kwa miaka 42.
Mawaziri hao wanachukua uongzi wa nchi ambayo haijakuwa na uongozi
thabiti kwa zaidi ya miaka 20 huku wababe wa kivita kutoka koo mbali
mbali, wapiganaji wa kiisilamu na nchi jirani za Somalia wote
wakipigania udbibiti wa Somalia baada ya kupindulia kwa aliyekuwa rais
Siad Barre mwaka 1991.
Changamoto kubwa
"Baada ya majidiliano ya muda mrefu na kushauriana , nimeteua baraza la mawaziri, ambalo linajumuisha mawaziri kumi. Miongoni mwao ni waziri wa kwanza mwanamke kwa mara ya kwanza katika historia ya Somalia’’ alisema waziri mkuu.
Bi Adan anatoka katika jimbo la Somaliland lililojitenga na ameishi nchini uingereza kwa miaka mingi.
"Uteuzi wangu kama waziri wa mambo ya nje
ni jambo la kihistoria kwa Somalia na hasa kwa wanawake , inafungua
ukurasa mpya wa siasa za nchini humo na tutafanikiwa katika uongzi wetu.’’ Alisema bi Adan
Changamoto kubwa inayokabili serikali mpya inayoungwa mkono na Umoja wa matifa, ni wapiganaji wa Al shabaab.
Licha ya kupoteza baadhi ya miji mikuu,
wanamgambo hao wangali wanadhibiti sehemu kubwa za kusini mwa Somali
pamoja na maeneo ya kati.
Al-Shabab wamefanya mashambulizi kadhaa ya
kujitoa mhanga mjini Mogadishu tangu kufurushwa kwao kutoka Mogadishu na
majeshi ya Muungano wa Afrika mwaka jana ikiwemo mashambulizi kadhaa
baada ya uchaguzi wa Rais Mohamud.