TASWIRA JINSI ULIVYOKUA WAKATI SHEIKH PONDA NA WENZAKE 49 WALIPOPANDISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Posted on
Nov 2, 2012
|
No Comments

Sheikh Ponda na pingu zake mikononi, akirejeshwa rumande.

Askari Magereza wa kutuliza ghasia, aliyejihami kwa silaha na vifaa vingine akiwa makini kulinda usalama

Polisi wa Mbwa nao walichukua nafasi yao

Askari wa kutuliza ghasia magerezani, nao walikuwepo kikamilifu

Askari
wa kutuliza ghasia magereza, akiwa ameshika lindo mbele ya mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Alhamisi Novemba 1, 2012

Polisi
wa Mbwa akifanya doria kwenye barabara ya Bitbi Titi mbele ya jengo la
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana

Polisi wa Mbwa wakisubiri amri ndani ya gari lao nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Novemba 1, 2012

Farasi
wa polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh Ponda, waliojikusanya
nje ya uzio wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Alhamisi Novemba 1, 2012

Kiongozi
wa Askari magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na wenzake, kutoka
mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa kwa kesi yao

Sheikh
Ponda Issa Ponda, akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba
cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi
Novemba 1, 2012.

Mshtakiwa akiwa amebebwa na mwenzake baada ya kudondoka mahakamani na kupoteza fahamu

Huiingii mahakama ya Kisutu bila ya kukaguliwa na mashine za kugundua vitu vya asili ya chuma hapo.
Sheikh Ponda msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu
anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la
Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu na kuiba
mali mbali mbali zenye thamani ya shilingi milioni 59, madai ambayo
washtakiwa wote waliyakanusha.
Hakimu huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba moja.
Ulinzi katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa kutuliza ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam.
Kikundi kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao wakatawanyika.
Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena