WASTAAFU WATUMIE OFISI ZA MIKOA NA KANDA KUCHUKUA MAFAO YAO- WAZIRI KABAKA
Posted on
Nov 9, 2012
|
No Comments
Waziri
wa Kazi na Ajira , Gaudencia Kabaka akijibu swali Bungeni mjini
Dodoma leo asubuhi juu ya kuwepo mikakati ya mifuko yahifadhi ya jamii
kuwapa wastaafu mafao yao bila usumbufu.
Wastaafu wameshauriwa
kutumia ofisi za mikoa na kanda kuchukua mafao yao badala ya utaratibu
uliozoeleka wa wa sasa kufuata mafao hayo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudencia Kabaka ameliambia Bunge leo wakati akijibu swali la Mbunge wa
Busanda (CCM), Lolesia Jeremiah Bukwimba.
Mbunge wa Busanda ,
Bukwimba alitaka kujua ni mikakati gani inayofanywa na serikali kwa
kushirikiana na mifuko ya jamiikuhakikisha kuwa wastaafu hao hawaendelei
kupata kero kwa kufuata mafao yao Dar es Salaam badala ya sehemu zao za
kazi .
Mbunge Bukwimba pia
alitaka kujua kwa nini wastaafu hawanufaiki na fedha zao wanazoweka
kwenye mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii kabla yakustaafu kama vile
kupata mikopo ya kujenga nyumba na shughulizingine.
Waziri Kabaka alisema kuwa
kwa sasa mifuko hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA) wameweka mikakati ya kuanzisha utaratibu mzuri wa kutoa mikopo
kwa wafanyakazi kupitia SACCOS zawafanyakazi.
Kabaka alitaja faida
nyingine kama kutoa mafao ya afya, gharama za shule na nyingine nyingi
zikiwa baadhi ya faida wazipatazo wafanyakazi kabla ya kustaafu kwao.
Baadhi
ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania na wageni wengine,
wakiwa Bungeni leo asubuhi kufuatilia kikao mjini Dodoma