ZAIDI YA WATU 200 WAJERUHIWA TUNISIA KUFUATIA MAANDAMANO YA WATU WASIOKUWA NA AJIRA
Posted on
Nov 29, 2012
|
No Comments
Zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa katika siku ya pili ya mapigano katika mji wa Siliana nchini Tunisia.
Iliwabidi
maafisa usalama kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za rashasha
kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakidai ajira, huku kukiwa na taarifa
za watu kujeruhiwa kwa risasi za moto.
Vyama vya wafanyakazi nchini humo vimeitisha maandamano zaidi.