KADI ZA MICHANGO YA HARUSI
Posted on
Dec 5, 2012
|
1 Comment
Ni kawaida kwa jamii yoyote duniani kuoa ama kuolewa na hasa
kwa binadamu aliyekamilika. Kimsingi kuoa ni jambo la heri kwa mtu kupata
mwenzi. Na ndugu jamaa na marafiki kuchangia kwa mawazo mali na misaada mingine
ya kijamii ili kufanikisha shughuli hiyo kukamilika.
Hata hivyo uchangiaji huu umekuwa wa kiholela mno, kwani waoaji na wanaoolewa ni vyema wakawa na utaratibu mzuri wa kugawa kadi hizo. Nasema hivi kwa sababu kuwa mgawa kadi anapaswa kufanya mawasiliano na mtu anayetaka ampe kadi kwa ajili ya kumchangia mchango huo. badala ya kuzigawa kadi hizo pasipo hiari ya mchangiaji, maana mgaw kadi unashangaa anakuletea kadi, ama anaibwaga mezani kwako kama ni ofisin au anawaachia watoto kama ni nyumbani.
Ombi langu kwa waoaji wote fanyeni mawasiliano kabla ya kugawa kadi maana sasa zimekuwa kero kiasi kwamba ndani ya mwezi mmoja unaweza kugawiwa kadi zisizopungua kumi na wote wantaka mchango usiopungua elfu hamsini. kwa namna hii hatuwezi kwenda kabisa.
Hata hivyo niwaombe watanzaia wenzangu tunahitaji kubadilika ili mitizamo yetu isilenge zaidi katika uchangiaji wa harusi, tunahitaji kuchangia zaidi katika elimu kwani kuna vijana wetu hawana hata dwati la kukalia, yatima, wajane na wenine wengi wenye mahitaji badala ya kuchangia harusi.
Kufanya harusi kubwa katika kumbi kubwa zenye kugharimu mamilion ya shilingi za kazi gani, kwani hazina tija kwa maendeleo ya taifa hili ambalo wananchi wake wako katiak wimbi la umaskini mkubwa.

weka sample ya kadi katika blog yako ili watu wajioneee kadi na kama kutakuwa na urahisi wa kudownlown basi watu wa pitie kwako.
ReplyDelete