KIBAKI AHUTUBIA TAIFA LA KENYA KWA MARA YA MWISHO KAMA RAIS
Posted on
Dec 13, 2012
|
No Comments
Sherehe
za mwaka huu za uhuru wa Kenya zilzo fanyika jana tarehe 12 Desemba ni
nafasi ya mwisho kwa Rais Mwai Kibaki kulihutubia taifa katika sikukuu
ya kitaifa hasa ikizingatiwa sikukuu nyingine ya kitaifa ni Siku ya
Madaraka itakayokuwa tarehe 1 Juni mwakani, ambapo atakuwa hayupo tena
madarakani.
Kenya
ilitumbukia katika ghasia zilizosababishwa na harakati za kuwania
madaraka kati ya rais Mwai Kibaki na Raila Odinga baada ya uchaguzi
mwaka 2008 kabla ya kufikiwa makubaliano yaliyosimamiwa na jopo maalum
la Kimataifa lililoongozwa na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa
Kofi Annan na hatimae kuundwa serikali ya muungano.
Machafuko
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 yalisababisha kiasi ya watu 1,100
kuuwawa na wengine zaidi ya 65,000 kupoteza makaazi yao.
Ikiwa
ni tukio lake la mwisho la kitaifa kuliongoza kabla ya kuondoka
madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Machi mwaka 2013, Rais Mwai
Kibaki ameitumi siku ya uhuru kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana
nchini humo tangu alipoingia madarakani miaka 10 iliyopita, kubwa zaidi
ikiwa ni ukuaji wa kiuchumi, maendeleo ya sekta ya miundo mbinu kutokana
na miradi iliyoanzishwa katika kipindi hicho cha utawala wake pamoja na
kupitishwa katiba mpya mwaka 2010
Katika
hotuba amewahimiza wananchi wa Kenya kutilia maanani umuhimu wa amani
na usalama na kuweka kando tofauti za kikabila katika uchaguzi mkuu ujao
huku pia akizungumzia juhudi za serikali katika kupambana na wanamgambo
wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia ambako jeshi la Kenya
linashirikiana na kikosi cha Umoja wa Afrika katika harakati hizo.