MISRI IKULU HAIKALIKI...
Posted on
Dec 6, 2012
|
No Comments
Vurugu
zimezuka katika mji mkuu wa Misri, Cairo, baina ya watu wanaomuunga
mkono Rais wa taifa hilo Mohammed Mursi na wapinzani kufuatia kutangazwa
kwa taarifa kuwa kura ya maoni inayohusu mswada wa katiba mpya
itafanyika kama ilivyopangwa ifikapo tarehe 15 ya mwezi huu.
Kauli
hiyo iliyotolewa na makamu wa Rais wa Misri Mahmud Mekki, imesababisha
vurugu kubwa nje ya Ikulu ambapo mahema yanayozunguka eneo hilo
yaliangushwa. Waandamanaji wamewasha moto mitaani, kurusha mawe pamoja
na mabomu ya petroli.
Maandamano
ya kumpinga Rais Mursi yameikumba Misri tangu kiongozi huyo ajipe
madaraka ya ziada wiki mbili zilizopita. Waandamanaji wamelazimika
kuondoka nje ya Ikulu na maeneo ya jirani kutokana na hali ya mapigano
kuwa mbaya zaidi.