WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA WAPEWA SIKU 30 KUZISALIMISHA
Posted on
Dec 6, 2012
|
No Comments
Serikali
imetoa siku 30 kwa wananchi wanaomiliki silaha kinyume na sheria
kuzisalimisha kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi (Pichani) wakati akizungumza na waandishi wa
habari
Dkt.
Nchimbi alisema kuwa na tatizo la kuzagaa na matumizi holela ya silaha
zinazomilikiwa isivyo halali lichangia matukio ya uhalifu ambayo
yamekuwa yakijitokeza sehemu mbalimbali nchini
Alisema
kuwa kwa mfano katika mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu kumekuwepo
na matukio ya ujambazi 876 ambayo yalisababisha vifo 138 vya raia na 6
vya askari.
Aidha
Dkt . Nchimbi aliongeza kuwa jumla ya mali zenye thamani ya shilingi
bilioni 4.5 zilizoibiwa kwa kutumia silaha zinazomilikiwa kinyume cha
sheria na zile zinazomilikiwa kisheria lakini wamiliki wake wanazitumia
katika uhalifu.
Aliongeza
kuwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu jumla ya
silaha 62 ziliibiwa kutoka kwa wamiliki wake halali na silaha 304
zilikamatwa katika matukio mbalimbali ya uhalifu
Kufuatia
hali hiyo Serikali imewaagiza watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha
Sheria kusalimisha silaha hizo katika vituo vya Polisi au wenyeviti wa
vitingoji , wakuu wa mikoa na wilaya.
Aidha
Dk. Nchimbi alisema kuwa kwa wale ambao muda utakamilika bila
kusalimisha silaha msako mkali utafanyika kuanzia tarehe 5 Januari
mwakani
Waziri
Nchimbi aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kutoa
taarifa zitakazosaidia kubaini uhalifu na makundi yaliyo katika jamii
yetu.