photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > WAZIRI MKUU WA MALI CHEIK MODIBO DIARRA AJIUZULU BAADA YA KUKAMATWA NA JESHI

WAZIRI MKUU WA MALI CHEIK MODIBO DIARRA AJIUZULU BAADA YA KUKAMATWA NA JESHI

Posted on Dec 11, 2012 | No Comments

 Waziri Mkuu wa Mali Cheik Modibo Diarra ametangaza kujiuzulu wadhfa wake katika televisheni ya taifa, saa chache baada ya kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na wanajeshi wanaosadikiwa kuhusika na mapinduzi yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.
Cheik Modibo Diarra alikamatwa nyumbani kwake katika mji mkuu wa Bamako, kwa kile kinachosemekana kuwa ni maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi hayo Kapteni Amadou Sanogo.
Waziri Mkuu huyo alikuwa akijiandaa kusafiri kuelekea Ufaransa.
Diarra alikamata madaraka ya Uwaziri Mkuu wa Serikali ya Mpito mwezi Aprili baada ya maafisa wa jeshi waliofanya mapinduzi kukabidhi madaraka mikononi mwa raia.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru