AKAUNTI YA YANGA YASHIKILIWA NA TRA
Posted on
Jan 8, 2013
|
No Comments
Kocha wa Yanga Kocha Ernest Brandts akisimamia mazoezi nchini Uturuki
WAKATI Shirikisho la Soka nchini (TFF) limepata
nafuu katika sakata la kodi kutoka kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA),
mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Yanga wamekumbana na
sakata linalofanana na hilo baada ya kufungiwa kwa akaunti zake za
benki.
Mwishoni mwaka jana, TRA ilifungia akaunti ya TFF
na baadaye kuchukua kiasi cha shilingi 157,407,968 kama malipo ya kodi
ya Llipa kwa Kkadri Uunavyopata (PAYE) baada ya shirikisho hilo
kushindwa kuwasilisha malipo ya makocha wake enzi ya Mbrazili, Marcio
Maximo.
Pamoja na mishahara ya makocha hao ilikuwa
inalipwa na serikali, TRA ilitekeleza wajibu wake na vilabu pamoja na
TFF kutangaza kutocheza ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguko wa pili kwani
fedha zilizochukuliwa zilikuwa za vilabu baada ya TFF kulipwa na
mdhamini wa lLigi hiyo, Vodacom Tanzania.
Baada ya mzozo wa muda mrefu, hatimaye juzi
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na
Michezo, Amos Makala alimaliza kutangaza kuwa sakati hilo na kuzitaka
limetatuliwa na hakuna sababu ya klabu kutegomea kuanza kwa Ligi Kuu ya
Tanzania Bara.
Sakata linalofanfana na hilo kwa sasa limeibukia
kwa klabu ya Yanga baada ya taarifa za uhakika za kufungwa kwa akaunti
yake ya benkdi ya CRDB namba 01J1095095801 na kuwapa usumbufu baadhi ya
wanachama waliokuwa wanataka kulipia ada ya uanachama ili waweze kuingia
mkutano mkuu wa Januari 19.
Mwananchi lilipozungumza na Kkatibu Mmkuu wa
Yanga, Laurence Mwalusako juu ya madai hayo hakukanusha wala kukubali
zaidi ya kusema akaunti za klabu hiyo ni za Yanga na si za watu wengine
wanaohitaji kuzifuatilia.
“Masuala ya akaunti ni yetu, wewe yanakuhusu nini,
kama zimefungiwa au hazijafungiwa wewe haikuhusu, hebu fanya mambo
yanayokuhusu, masuala ya akaunti za Yanga achana nayo, kwanza sitaki
kuulizwa juu ya kufungiwa kwa akaunti hizo sababu ziko juu ya uwezo
wangu kulijibu naomba uniache,” alisema Mwalusako.
Aidha, Mwalusako alipoulizwa juu ya baadhi ya
wanachama kulalamikia kitendo cha akaunti hizo kufungiwa alijibu kwa
kifupi kama wanalalamika waende wakalalamike kwao Yanga na si kwenye
vyombo vya habari.
Baadhi ya wanachama hao walisema kuwa wanapata
usumbufu na wala hawajui hatima yake kwani sakati hilo kwa sasa limedumu
kwa wiki kadhaa.
Walisema kuwa baada ya kuwasiliana na viongozi,
walijibu kuwa wapo katika hatua za mwisho za kuhakikisha akaunti hiyo
inafanya kazi kama kawaida bila ya kusema kiini cha tatizo.
Wanachama hao waliutaka uongozi kutangaza wazi
kiini cha tatizo hilo na lini litaisha kwani wanapoteza muda wao kupanga
foleni benki na wakifika wakatli wa malipo wanaambiwa akaunti hiyo
imefungwa.
“Waseme nini tatizo na tatizo hilo litaisha lini,
usumbufu ni mkubwa na sisi wanachama tuna morali ya kulipia kadi zetu
ili tuweze kuingia katika mkutano, morali inashuka na kibaya zaidi,
tunapoteza muda,” alisema mmoja wa wanachama hao.wa klabu hiyo
aliyekataa kutajwa jina lake.
Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Ligi alikiri kuwepo kwa tatizo hilo, huku akisisitiza klabu zifuate taratibu za malipo, kuajili na mambo mengine ili kuepukana na usumbufu.
Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Ligi alikiri kuwepo kwa tatizo hilo, huku akisisitiza klabu zifuate taratibu za malipo, kuajili na mambo mengine ili kuepukana na usumbufu.