photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > ASKARI, RAIA MATATANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

ASKARI, RAIA MATATANI KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

Posted on Jan 7, 2013 | No Comments


ASKARI polisi wawili na raia mmoja kutoka Biharamulo na Bukoba wanashikiliwa na polisi wilayani Serengeti kwa tuhuma za kukutwa na vipande 17 vya meno ya tembo.
Tukio hilo lililothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, lilitokea jana katika Kijiji cha Rwamchanga na mjini Mugumu askari mmoja mtuhumiwa ni mpelelezi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai  mjini Bukoba na mwingine ni wa Ofisi ya Upelelezi Biharamulo.
Askari hao walikamatiwa katika nyumba moja ya kulala wageni iliyoko mjini Mugumu, usiku wa kuamikia jana baada ya mwenzao kukamatwa na shehena hiyo na kuwapeleka askari walikokuwa  wenzake .
Kamanda Kwakyoma alisema askari hao walikiri kuwa walifika Mugumu kwa maelekezo ya mfanyabiashara mkazi wa Biharamulo.
Kukamatwa kwao kunatokana na taarifa zilizotolewa na Tanapa kwa polisi kuhusu mtandao unaundwa  na wafanyabiashara wakubwa na baadhi ya watendaji wa vyombo vya dola kwa ajili ya kufanya hujuma dhidi ya wanyamapori.
Kwa mjibu wa kamanda askari hao tayari wameshawasomea mashtaka ya kijeshi kabla ya kufunguliwa mashtaka katika mahakama za kiraia.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru