MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012
Posted on
Jan 11, 2013
|
No Comments
1.0 UTANGULIZI
Mtihani
wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote
kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012. Mwaka 2012
kulikuwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, ikiwa ni
ongezeko la vituo 117(2.79 %) ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.
2.0 WATAHINIWA WALIOSAJILIWA, WALIOFANYA NA WASIOFANYA MTIHANI
2.1 Idadi
ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao
wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851. Idadi hii ni upungufu wa
watahiniwa 36,240 (7.76%) ikilinganishwa na mwaka 2011 ambapo walikuwa
466,567.
2.2 Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027.
2.3 Watahiniwa
44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana
ni 18,231 na wavulana 25,825. Mwaka 2011 watahiniwa 47,527(10.19%)
hawakufanya mtihani. Sababu za watahiniwa kutofanya mtihani ni pamoja na
utoro, kuugua, kudaiwa ada, kufukuzwa shule, mimba na vifo.
3.1 Watahiniwa
waliofaulu ni 249,325 (64.55 %) kati yao, wasichana ni 113,213 na
wavulana 136,112. Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 19.15
kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011. Watahiniwa waliofaulu kwa kiwango cha
A, B, na C walikuwa 127,981 (33.13%) na waliofaulu kwa kiwango cha D ni
121,344 (31.42%). Alama ya juu ya ufaulu ni 92%
3.2 Wastani wa ufaulu kwa masomo ni 38%, wastani huu umepanda kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwaka 2011 ambapo ulikuwa 31%.
3.3 Watahiniwa
136,923 (35.45 %) hawakufaulu mtihani, wakiwemo wasichana 74,020 na
wavulana 62,903. Watahiniwa hawa watalazimika kukariri kidato cha pili
mwaka 2013. Aidha, mwaka 2011 watahiniwa 228,759 (54.59%) hawakufaulu
mtihani.
3.4 Watahiniwa 23 matokeo yao yamefutwa kutokana na tuhuma za udanganyifu. Watahiniwa hawa wanatoka katika shule zifuatazo;
Na
|
Jina la Shule
|
Kanda
|
Idadi ya watahiniwa
|
1.
|
Kiyongwire
|
Mashariki
|
2
|
2.
|
Nyashishi
|
Ziwa
|
4
|
3.
|
Thaqaafar
|
Ziwa
|
3
|
4.
|
Paroma
|
Ziwa
|
2
|
5.
|
Murangi
|
Ziwa
|
1
|
6.
|
Bukene
|
Magharibi
|
7
|
7.
|
Kili
|
Magharibi
|
1
|
8.
|
Binza
|
Magharibi
|
1
|
9.
|
Kizumbi
|
Magharibi
|
1
|
10.
|
Kolandoto
|
Magharibi
|
1
|
Watahiniwa hawa nao watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013.
4.0 UFAULU KWA SHULE
4.1 Shule Zilizoshika Nafasi Kumi za Mwanzo
4.1.1 Shule za Serikali
NA.
|
SHULE
|
KANDA
|
1.
|
MZUMBE
|
MASHARIKI
|
2.
|
TABORA WAVULANA
|
MAGHARIBI
|
3.
|
ILBORU
|
KASKAZINI MAGHARIBI
|
4.
|
KIBAHA
|
MASHARIKI
|
5.
|
IYUNGA
|
NYANDA ZA JUU
|
6.
|
MSALATO
|
KATI
|
7.
|
MALANGALI
|
NYANDA ZA JUU KUSINI
|
8.
|
IFUNDA UFUNDI
|
NYANDA ZA JUU KUSINI
|
9.
|
SAMORA MACHEL
|
NYANDA ZA JUU
|
10.
|
KILAKALA
|
MASHARIKI
|
4.1.2 Shule Zisizo za Serikali
NA.
|
SHULE
|
KANDA
|
1.
|
KAIZIREGE
|
ZIWA MAGHARIBI
|
2.
|
MARIAN WAVULANA
|
MASHARIKI
|
3.
|
ST. FRANCIS
|
NYANDA ZA JUU
|
4.
|
DONBOSCO
|
NYANDA ZA JUU KUSINI
|
5.
|
BETHEL SABS
|
NYANDA ZA JUU KUSINI
|
6.
|
MARIAN WASICHANA
|
MASHARIKI
|
7.
|
DON BOSCO (MOSHI)
|
KASKAZINI MASHARIKI
|
8.
|
CANOSSA
|
DSM
|
9.
|
ST. JOSEPH ITERAMBOGO SEM.
|
ZIWA MAGHARIBI
|
10.
|
CARMEL
|
MASHARIKI
|
4.2 Shule zilizoshika nafasi kumi za Mwisho
4.2.1 Shule za Serikali
NA
|
SHULE
|
KANDA
|
1.
|
MIHAMBWE
|
KUSINI
|
2.
|
DINDUMA
|
KUSINI
|
3.
|
KIROMBA
|
KUSINI
|
4.
|
MARAMBO
|
KUSINI
|
5.
|
MBEMBALEO
|
KUSINI
|
6.
|
KINJUMBI
|
KUSINI
|
7.
|
LITIPU
|
KUSINI
|
8.
|
LUAGALA
|
KUSINI
|
9.
|
MIGURUWE
|
KUSINI
|
10.
|
NAPACHO
|
KUSINI
|
4.2.2 Shule Zisizo za Serikali
NA.
|
SHULE
|
KANDA
|
1.
|
MFURU
|
MASHARIKI
|
2.
|
PWANI
|
MASHARIKI
|
3.
|
DORETA
|
KATI
|
4.
|
KIGURUNYEMBE
|
MASHARIKI
|
5.
|
RURUMA
|
KATI
|
6.
|
AT-TAAUN
|
MASHARIKI
|
7.
|
JABAL HIRA SEM
|
MASHARIKI
|
8.
|
MKONO WA MARA
|
MASHARIKI
|
9.
|
KILEPILE
|
NYANDA KUSINI
|
10.
|
KIUMA
|
NYANDA KUSINI
|
5.0 UFAULU WA WANAFUNZI
Wanafunzi Walioshika Nafasi Kumi za Mwanzo
Na
|
JINA
|
JINSI
|
SHULE
|
1.
|
MAGRETH KAKOKO
|
KE
|
ST FRANCIS
|
2.
|
QUEEN MASIKO
|
KE
|
ST FRANCIS
|
3.
|
LUKUNDO MANASE
|
ME
|
KAIZIREGE
|
4.
|
FRANK J NYANTARILA
|
ME
|
KAIZIREGE
|
5.
|
GRACE MSOVELLA
|
KE
|
ST FRANCIS
|
6.
|
HARIETH MAKIRIYE
|
KE
|
ST FRANCIS
|
7.
|
ROBINNANCY MTITU
|
KE
|
ST FRANCIS
|
8.
|
HUMRATH LUSHEKE
|
KE
|
ST FRANCIS
|
9.
|
MUKHSIN HAMZA
|
ME
|
KAIZIREGE
|
10.
|
ANASTAZIA KABELINDE
|
KE
|
KAIZIREGE
|
6.0 HITIMISHO
Matokeo
ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012,
yanaonesha kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka
2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012. Aidha, watahiniwa 249,325
wataendelea na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2013. Napenda kuwapongeza
wanafunzi wote waliofaulu kuendelea na masomo na kuwataka kuendelea na
bidii katika kujifunza.
Kwa
upande mwingine, watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa
ufaulu wa alama 30 na wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na
udanganyifu watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Ni vema
ikaeleweka kuwa kukariri kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine
kwa mwanafunzi kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya
sekondari kidato cha kwanza na cha pili kwa kiwango kizuri. Hivyo ni
matumaini yangu kuwa wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na
kuzingatia masomo ili waweze kufaulu, pia walimu kuwasaidia Wanafunzi
hao waweze kufanya vizuri.
Serikali
kwa upande wake itaimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi ya shule na
kuziwezesha shule kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuboresha
mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni pamoja na walimu
kubadili mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji na wazazi kufuatilia
maendeleo ya wanafunzi.
Vilevile,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi chini ya Mpango wa Maendeleo ya
Elimu ya Sekondari (MMES) itaendelea na jitihada zake za kuimarisha na
kuboresha mazingira ya utoaji elimu bora kwa kujenga maabara za
sayansi, kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu, kununua vifaa vya
kufundishia na kujifunzia na kuimarisha usimamizi wa shule. Aidha,
wizara itaendelea kutoa walimu kwa awamu kila mwaka ili kukabiliana na
upungufu uliopo.
Mhe. Philipo Mulugo (Mb)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
11/01/2013