MBUNGE ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI HUKU AKINYESHEWA NA MVUA
Posted on
Jan 5, 2013
|
No Comments
Mbunge huyo ambae awali kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi alipewa mwamvuli kwa ajili ya kujikinga na mvua iliyoanza kunyesha muda mfupi kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi hao ,baadae alikataa kujifunika mwamvuli huo kwa madai kuwa hawezi kujifunika mwamvuli kula starehe wakati wananchi wake wanakero na wananyeshewa na mvua.
Kutokana na hali hiyo mbunge huyo aliendelea kusikiliza na kujibu maswali mbali mbali ya wananchi juu ya ufisadi unaofanywa na viongozi wa kata hiyo kwa kushindwa kusoma mapato na matumizi wala kuitisha mkutano kijijini hapo.
Wananchi hao mbali ya kumpongeza mbunge huyo kwa kuonyesha mfano kwa viongozi wengine kwa kufika kulala katika kijiji hicho na kusikiliza kero zao ,bado walisema kuwa viongozi wa kijiji hicho na kata wamekuwa ni tatizo kubwa na wao kama wananchi wameonyesha kuwachoka viongozi hao.
Akizungumza katika mkutano huo mbunge Filikunjombe alisema kuwa anasikitishwa na utendaji wa viongozi wa kata hiyo kwa kushindwa kufanyia kazi matatizo ya wananchi wa kijiji hicho hata kwa kushindwa kujenga choo cha wanafunzi .
Hata hivyo alisema kuwa ofisi yake anachukua hatua ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya Msingi Chanjale