KWELI NDOA INATAKA MOYO...
Posted on
Feb 18, 2013
|
No Comments
Ndugu zanguni yamenikuta na naomba ushauri
wenu,Mimi ninaishi na mume wangu yapata miaka miwili sasa,nina mpenda sana Mume
wangu na ninaamini kuwa naye ananipenda pia.Ila kuna tatizo linanisumbua sana
juu yake ambalo linanipa wasiwasi kiasi kwamba nashindwa kuelewa hatma ya
mahusiano yetu ya ndoa kwa maana ya kwamba nahofia yasije yakaingia shubiri na
ile imani nlionayo juu yake ikateteleka.Ni hivi kabla ya kunioa mimi aliwahi
kuwa na mahusiano na wanawake wengine ila mwanamke wa mwisho ambaye aliachana
nae amekua akiendelea kuwasiliana na mume wangu na kila ninapohoji juu ya hilo
Mume wangu hunijibu kuwa hauna kitu kinachoendelea baina yetu ni rafiki yangu
tu wakawaida na hana shida yoyote na sisi kwanza huwa anapiga simu na kutuma
meseji za kutujulia hali,anyways nimejitahidi sana kuwa na mtizamo chanya na
kuuambia moyo wangu uamini hivyo.Ila siku zinavyokwenda nikaona mazoea yanakua
sio mazuri kwa maana wakati mwingine humpigia simu ana hutuma meseji humueleza
mume wangu kuwa amemmiss sana na anataka kuonana nae na vitu kama
hivyo.Nlimwambia mume wangu mawasiliano na huyo mpenzi wako wa zamani
hayanibariki hata kidogo naomba uwe na mipaka na ikibidi uache kwa maana
yananiumiza mimi zaidi,aliniahidi kufanya hivyo na kweli kwa kipindi fulani
kazi ilipungua ila sasa leo ametuma tweets kuhusu mume wangu kwenye mtandao wa
twitter kitu ambacho kimeniuma maana anaeleza jinsi anavyofurahia tendo la ndoa
na mume wangu na baada ya kuliona hilo nkampigia mume waqngu kumweleza
akaniambia atampigia simu kumsema juu ya hilo na kumuonya.Badala yake
kilichotokea yule mwanamke alituma tweets za kunitukana na kunidhalilisha mimi
kitu ambacho kinaniuma sana kwa maana mume wangu anasema yule mwanamke ni
rafiki mzuri tu na hana shida hata kidogo.Nisaidieni ushauri ndugu zangu je
niendelee kuvumilia hayo yote yanayojitokeza na kuamini maneno ya mume wangu
kuwa huyo mwanamke hana shida na sisi ama nifanyenye?Naomba ushauri wenu katika
hili.....