MKAPA KUONGOZA MAZISHI YA ASKOFU MSARIKIE
Posted on
Feb 14, 2013
|
No Comments
Huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Maaskofu wanapofariki kuzikwa ndani ya kanisa.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa anatarajiwa kuungana na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali katika ibada ya mazishi ya Askofu huyo mstaafu wa Jimbo la Katoliki Moshi.
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa anatarajiwa kuungana na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali katika ibada ya mazishi ya Askofu huyo mstaafu wa Jimbo la Katoliki Moshi.
Viongozi wanaotajwa kuhudhuria mazishi hayo ni
pamoja na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Stephen
Wassira, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na zaidi ya
maaskofu 25 kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Wengine watakaoshiriki katika mazishi hayo ni
pamoja na maaskofu, watawa, mapadri, waumini na viongozi wa madhehebu
mengine ya dini.
Mhashamu Askofu Isaac Amani Masawe aliiambia
Mwananchi jana kuwa mwili wa Marehemu Msarikie (82) ulisafirishwa kwa
ndege jana ukitokea Nairobi.
Watu mbalimbali walianza kutoa heshima za mwisho kuanzia jana mchana hadi leo.
Ibada ya mazishi ya Mhashamu Askofu Msarikie aliyefariki katika Hospitali ya Nairobi ilipangwa kuanza saa nne asubuhi leo kanisani hapo .
Ibada ya mazishi ya Mhashamu Askofu Msarikie aliyefariki katika Hospitali ya Nairobi ilipangwa kuanza saa nne asubuhi leo kanisani hapo .
Alisema Marehemu huyo aliyestaafu mwaka 2007
aliugua ugonjwa wa saratani takribani kwa wiki sita na kupelekwa Nairobi
kwa matibabu zaidi na baadaye kufariki dunia akiwa huko.
Askofu Masawe alisema Marehemu aliteuliwa kwenye Daraja la Uaskofu Mei Mosi, 1986 anasifika kama kiongozi aliyependa maendeleo katika sekta tofauti kama vile Afya, Elimu na Kilimo ambapo hata kabla hajapelekwa hospitalini ugonjwa ulimkuta akiwa shambani akimwagilia migomba ya ndizi shambani kwake Kilema Wilaya ya Moshi Vijijini.

Askofu huyo anakuwa wa Askofu wa pili kuzikwa kanisani hapo baada ya askofu wa kwanza Joseph Sipendi kuzikwa mwaka 1985.