MUHIMBILI WAFAFANUA CHANJO YA UKIMWI
Posted on
Feb 17, 2013
|
No Comments
JOPO la Madaktari wa Chuo wa Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), wametoa ufafanuzi kuhusu majaribio
ya chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi, wakisema bado wanaendelea kuifanyia
utafiti zaidi.
Kiongozi wa Jopo la Madaktari hao lililofanya
utafiti huo, Profesa Muhammad Bakari aliliambia gazeti hili kuwa ingawa
majaribio ya chanjo hiyo yaliyofanyika nchini mwaka 2007-2010 na
2008-2012, yameonyesha mafanikio mazuri, lakini majaribio hayo
hayajafikia hatua ya kupatikana kwa chanjo kamili.
Alisema majaribio hayo, yamethibitisha kuwa chanjo
ya DNA - MVA ilikuwa salama na yenye uwezo wa kuufanya mwili utengeneze
kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi (VVU).
Profesa Bakari ambaye pia ni Naibu Makamu Mkuu
Chuo cha MUHAS, alisema baada ya kuanza kufanya utafiti, jopo la
madaktari bado liliendelea na utafiti zaidi, ulioanza mwaka 2008 hadi
2012 ili kupata chanjo.
“Hatukuishia hapo, utafiti wa pili (TAMOVAC-01),
ulifanyika kati ya mwaka 2008 na mwaka 2012. Utafiti huu ulijumuisha pia
nchi jirani ya Msumbiji.
Alisema utafiti wa awali ambao ulijulikana kama
HIVIS-03, ulihusisha askari 60 ambao walifuatiliwa kwa karibu wakati
wote wa utafiti ili kuhakiki usalama wa chanjo na uwezo wa chanjo kute
ngeneza vichocheo vya kinga dhidi ya VVU.
Juhudi za kukabiliana na VVU zimekuwa zikifanywa
na wanasayansi mbalimbali duniani lengo likiwa ni kupata chanjo ama dawa
ya kutibu. Kwa sasa waathirika wamekuwa wakitumia dawa za kupunguza
makali ya Ukimwi (ARV).