NZEGA WADAIWA KUIBA MAHINDI YA MSAADA
Posted on
Feb 7, 2013
|
No Comments
KUFUATIA kuanza ugawaji mahindi ya msaada
wilayani Nzega mkoani Tabora ili kupunguza tatizo za njaa, viongozi
wanne akiwepo na diwani wa kata ya Mwamala, anadaiwa kushikiliwa na
Polisi kwa tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya gunia 39 za mahindi.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bituni
Msangi kuwa, viongozi hao wanakabiliwa na tuhuma hizo za wizi wa mahindi
gunia 39 ya Kata ya Mwamala ambapo mahindi hayo yalipotea.
Msangi akizungumza na gazeti hili jana, alisema
kuwa tukio hilo lilitokea Januari 29, mwaka huu baada ya taarifa hizo
kufika ofisini kwake kutoka kwa wananchi wasamaria wema juzi.
Alisema kuwa, wananchi hao ambao majina yao
yamehifadhiwa walitoa taarifa hiyo na hatua za ufuatiliaji zilianza
katika kata hiyo ya Mwamala ambapo uchunguzi wa awali ulibani kuwa,
viongozi hao akiwemo diwani wa kata hiyo wanatuhumiwa kuhusika na
ubadhilifu huo.
Alisema wanatuhumiwa na ubadhilifu huo ni pamoja
na diwani wa kata hiyo,Mtendaji wa kijiji, mwenyekiti wa kijiji(majina
yanahifadhiwa), pamoja na mlinzi.
Alisema kuwa, watuhumiwa wengine wanaotafutwa
kuhusika na tukio hilo kuwa ni pamoja na kaimu mtendaji wa kijiji,
mlinzi mwingine na dereva wa roli lililobeba shehena hiyo.
Mkuu huyo aliliambia gazeti hili kuwa, kata hiyo
ilipaswa kupokea magunia 193 sawa na tani 18 hata hivyo magunia ya awali
yaliyo pelekwa yalikuwa magunia 130 ambapo magunia hayo yalipohesabiwi
na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya walikuta magunia 91.
Msangi alisema kuwa mahindi hayo hayakupokewa na
kamati ya maafa, haikupata taarifa kuwa mahindi yamefika na kuongeza
kuwa viongozi hao hawakupaswa kupokea mahindi hayo bali walipaswa kuwa
waangalizi tu.
Aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea ilikubaini mahindi yaliyopotea na kuwapata washiriki wengine zaidi.
Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa
viongozi wa wilaya pale wanapokuwa na mashaka ya utekelezaji wa
maihindi hayo, pamoja na kuwahimiza viongozi wa ngazi za kata na vijiji
kutambua wajibu wao.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,
Rozalia Magoti alisema kuwa kamati husika zigawe mahindi hayo huku
viongozi wa kata na vijiji wakisimamia zoezi hilo.
Alisema kuwa viongozi hao wanapaswa kutopa taarifa
za kila siku za ugawaji wa mahindi hayo ikiwa na ugawaji wa uangalifu
ili zoezi hilo lifanikiwe.
Magoti amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kutoa taarifa hizo na kutoa ushirikiano kwa viongozi wa kata na vijiji na kuongeza kuwa uchunguzi wa polisi unaendelea ili kupata ukweli zaidi katika suala hilo. Tatizo la njaa limekumba maeneno na serikali inafanya jithada kuokoa hali hiyo
Magoti amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kutoa taarifa hizo na kutoa ushirikiano kwa viongozi wa kata na vijiji na kuongeza kuwa uchunguzi wa polisi unaendelea ili kupata ukweli zaidi katika suala hilo. Tatizo la njaa limekumba maeneno na serikali inafanya jithada kuokoa hali hiyo