JK AWAPA POLE WA VENEZUELA, UCHAGUZI BAADA YA SIKU 30
Posted on
Mar 6, 2013
|
No Comments
Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Venezuela kutokana na kifo cha rais wa nchi hiyo, Hugo Chavez.
Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema kifo cha Chavez ni pigo kubwa na yeye binafsi ataendelea kumkumbuka kutokana na uhodari wake wa kutetea mataifa madogo yanayoinukia kiuchumi.
Rais Chavez aliyeongoza taifa lake kwa mihula miwili, alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ya tumbo iliyogundulika mwaka 2011, na tangu wakati huo alipatiwa matibabu ya mara kwa mara nchini Cuba.
Rais Kikwete alisema, dunia imepoteza kiongozi aliyekuwa hodari kutetea masilahi ya wanyonge na wakati wote alikuwa mstari wa mbele kusimamia kile alichokipigania.
Alisema yeye binafsi alivutiwa na utendaji kazi wa rais huyo ambaye alidai kumfahamu kwa kipindi kirefu.
Wakati huohuo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Elias Jasua ametangaza kuwa uchaguzi wa kiti cha Rais utafanyika ndani ya siku 30 zijazo.
Kiongozi huyo hakuweza kuapishwa baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana, baada ya hali yake ya kiafya kutetereka.
Uchaguzi utakaofanyika utakuwa ni wa pili ndani ya kipindi cha miezi sita, baada ya uchaguzi huo wa Oktoba ambao Chavez alishinda kiti hicho cha urais kwa mara ya nne mfululizo.
Jasua, alitangaza kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro atashika nafasi ya urais hadi uchaguzi utakapofanyika.
Maduro, alitangaza siku saba za maombolezo katika nchi hiyo. Katika uchaguzi huo, Maduro anatarajiwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama tawala cha PSUV.
Mpinzani mkubwa wa Chavez ambaye alibwagwa katika uchaguzi wa Oktoba, Henrique Capriles, aliitaka Serikali kuchukua hatua makini katika uchaguzi huo kulingana na katiba ya nchi hiyo.
Maradhi ya Chavez
Juni 2011, Chavez aligundulika kuwa na maradhi ya saratani. Hata hivyo Serikali haikuweka wazi ni saratani ya aina gani iliyokuwa ikimsumbua rais huyo.
Chavez alikwenda Cuba kwa matibabu ya mionzi na upasuaji ambayo hata hivyo hayakuwa na mafanikio mazuri.
Maradhi ya Chavez hata hivyo yalijirudia mapema mwaka jana na alirudi tena Cuba kwa matibabu.