MAMIA WAMUAGA MTANZANIA ALIYEUWAWA NCHINI CHINA.
Posted on
Apr 5, 2013
|
No Comments
MAMIA ya waombolezaji wamehudhuria mazishi ya Mtanzania aliyeuwawa China, takriban mwaka mmoja uliyopita, tukio lililowashangaza wengi na kujitokeza eneo la Mabatini, wilayani Ilemela ili kuaga mwili wa marehemu.
Ndugu, jamaa na marafiki wameonekana wakiwa na sura zenye simanzi na maswali mengi yasiyokuwa na majibu, kuhusiana na mazingira ya kifo cha Mkumbwa John Shayo, (37) mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza.
Baadhi ya waombolezaji wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mkumbukwa Joseph.
Mwili huo wa marehemu uliowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Machi 30, umeshuhudiwa na mwandishi wa habari hizi kutokuwa na jicho moja, jambo ambalo limewasikitisha waombolezaji hao na mmoja wa ndugu kupoteza fahamu wakati wa kuuaga.
Kwa mujibu wa maelezo ya mjomba wa marehemu, Erasto Kombe, baada ya mazishi hayo yaliyofanyika eneo la Kangai, hapa Ilemela, ndugu watakaa kikao na kuamua juu ya hatua watakayochukua dhidi wa wahusika wa kifo cha Mkumbukwa.
Utata umegubika mazingira ya kifo hicho, wakati mkewe, Neema Majukano akidai kuwa alipigiwa simu na Polisi wa China kuwa mumewe alikutwa amekufa katika Hoteli ya Milado, jijini Hong Kong, wengine wanadai kuwa marehemu alikutwa na mauti akisafirisha dawa za kulevya. Mamlaka nchini China ililazimika kuutunza mwili huo, mpaka ndugu wa marehemu walipojitokeza na kuusafirisha mpaka Tanzania.