photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > UFAHAMU UTAJIRI WA WEMA SEPETU...

UFAHAMU UTAJIRI WA WEMA SEPETU...

Posted on Apr 4, 2013 | No Comments



Well, well, well! Hiki ni kitu ambacho kila mmoja anapenda kukifahamu. Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu. So hebu tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya kuanzia mwezi June, 2012.

IMG_4951
1. Thamani ya nyumba yake

Wema Sepetu aliwaacha hoi watu wengi baada ya kuonesha nyumba yake mpya exclusively kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alisema thamani ya nyumba yake hiyo ilifikia shilingi milioni 400 na hiyo ni tofauti na karibu shilingi milioni 30 za kuipamba ndani. Hiyo ilikuwa ni tarahe za mwanzo za mwezi June, 2012.

Sebule
sebule


Wema Sepetu akielezea jambo
Wema Sepetu akielezea jambo

Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV
Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV

912
Sehemu ya nje ya nyumba

Sehemu ya nje ya nyumba
616
Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo
Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo

2. Uzinduzi wa filamu yake Superstar 
Katika historia ya Bongo Movies, hakuna filamu iliyowahi kuwa na uzinduzi wa nguvu kama wa filamu ya Wema ambayo hata hivyo haijawahi kutoka, Supastar. Katika uzinduzi huyo, Wema alimdondosha muigizaji namba moja wa kike nchini Nigeria, Omotola Jalade ambaye alimpeleka kwenye event iliyofanyika Giraffe Hotel Ocean View ambako watu mbalimbali walikutana kubadilishana mawazo na Omotola. Hiyo ilikuwa ni baada ya kushindwa kufika kwa wakati.

IMG_6117Awali ulifanyika uzinduzi wa filamu hiyo yenye mastaa kibao akiwemo yeye mwenyewe, TID, Shetta, Mwinyi Machozi, Chaz Baba, Barnaba na wengine kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro ambako mastaa wote wa orodha A nchini walihudhuria huku Shaa na Shilole wakiwa miongonimwa wasanii waliotumbuiza.DSC_0075
Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ben Kinyaiya na Irene Uwoya
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria
Ray, Dr Cheni, Steve Nyerere nao walihudhuria
DSC_0172


Shughuli nzima hiyo iliyofanyika mwishoni mwa mwezi June mwaka jana, ilitumia takriban shilingi milioni 40 zikiwemo gharama za kumlipa Omotola.

3. Gari anayomiliki
Kwa sasa Wema anamiliki gari aina ya AUDI Q7 ambayo thamani yake inafikia shilingi milioni 80. Awali ya hapo alikuwa na Toyota Mark X ambayo thamani yake ni takriban shilingi milioni 60.
Wema akiwa na mkoko wake
Wema akiwa na mkoko wake

4. Thamani ya ofisi na kampuni yake, Endless Fame Films
February 21, Wema alifanya uzinduzi maalum wa ofisi za kampuni yake ya Endless Fame Films zilizopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambazo thamani yake ni takriban shilingi milioni 70.
DSC_1824
off12-600x600

5. Gharama anayotumia kuwatunza mbwa wake, Vanny na Gucci 
Mtandao wa Global Publisher jana uliandika, “KWA wale wenye hali ngumu kimaisha wataishia kusema; ni kufuru iliyoje kwani staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amewafanyia mbwa wake wawili ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh. milioni 6.5 za madafu).

Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.

Akizungumzia ‘shopping’ hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar, Wema alisema: “Kiukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu utawakuta ndiyo maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake siwezi kuwa na amani.
0caeb4ac921811e28e6622000a9f0a1a_7
Vanny na Gucci wakicheza
Vanny na Gucci wakicheza
83b019e2914b11e28e0922000a9f1335_7
818e18e0921c11e2af9022000a1f9a23_7
90197700921811e2996f22000a1fbc6f_7
Vanny
Vanny
Vanny
Vanny
Gucci akiwa amelala
Gucci akiwa amelala

“Najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu.”

Leo kupitia Instagram, Wema ameandika, “Vanny ake heading to da hospital…. my poor baby is sick…. nat happy at all, hope u get better soon.”

6. Shilingi milioni 13 alizomtolea Kajala baada ya kusomwa hukumu yake 
Jana Wema Sepetu alimake headline baada ya kutoa mfukoni mwake shilingi milioni 13 kulipa faini aliyopigwa muigizaji mwenzie Kajala Masanja aliyehukumiwa jana kwenda jela miaka mitano ama kulipa kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza exclusively na Bongo5, Wema amesema hakufikiria mara mbili kutoa kiasi hicho cha fedha.
“Kusema kweli wanasemaga kwamba kutoa ni moyo so naamini what I did is best, nimetoa kwasababu I had to do it and sikuthink twice kuhusu kufanya hivyo,” amesema Wema.


“Nimefanya kama namsaidia rafiki yangu kama namsaidia ndugu yangu na sidhani kama ingekuwa ni kitu kizuri kumuona mwenzako anaingia kwenye dhahama, kwenye tabu, kwenye mateso na wakati nina uwezo wa kumsaidia kwahiyo I just did what I had to do.”


7. Jinsi anavyomwaga hela kwenye sherehe mbalimbaliKatika katika sherehe za 8020 Fashion’s Woman Celebration zilizofanyika kwenye siku ya wanawake duniani, Wema aliuteka ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kumwaga mihela kwa mwimbaji maarufu wa Taarabu nchini, Khadija Omar Kopa. Wema alimwaga mkwanja huo kumpongeza Khadija kwa kukonga moyo wake. Hayo ni machache tu tunayofahamu na kwa hesabu hizo bila shaka utakubaliana nasi kuwa Wema Sepetu ana mkwanja mrefu!!! 

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru