photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUFUNGULIWA ALHAMIS 23/05/2013

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUFUNGULIWA ALHAMIS 23/05/2013

Posted on May 20, 2013 | No Comments

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA 

TAARIFA YA KUFUNGUA CHUO 

 Chuo cha Uhasibu Arusha kinawatangazia Wanafunzi wote wa kozi za ngazi ya Cheti hadi Stashahada ya Uzamili kwamba chuo kitafunguliwa siku ya Alhamisi tarehe 23 Mei, 2013. Kuanzia tarehe 23 hadi tarehe 27 Mei, 2013 kutakuwa na zoezi la usajili katika lango kuu la kuingia chuoni kwa kuzingatia masharti yafuatayo: 

1. Kila Mwanafunzi aliyeomba upya kujiunga na chuo anapaswa kuonyesha kitambulisho chake cha chuo.

2. Kila Mwanafunzi aje na risiti au “Bank pay in slip” ya kuonyesha malipo ya karo na fedha zote anazodaiwa na chuo. 

3. Kila Mwanafunzi anapaswa kuingia mkataba mpya na Chuo. Mkataba huo unapaswa kusainiwa kabla Mwanafunzi hajasajiliwa. 

4. ANGALIZO: Hakutakuwepo na usajili baada ya tarehe 27 Mei, 2013. 

Mkuu wa Chuo

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru