KANISA LA TAG LACHOMWA MOTO MJINI TANGA
Posted on
May 18, 2013
|
2
Comments
Kanisa la TAG mjini Tanga limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo tarehe 18/5 na kuteketea kabisa. Pamoja na kanisa hilo kituo cha mafunzo ya watoto wadogo kilichokuwa jirani na kanisa nacho pia kimeteketezwa kwa moto. Pamoja na kwamba majirani wanatoa ushuhuda kwamba waliwasikia kikundi cha watu eneo hilo, mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Source: star Tv
ndo tulipofikishwa na serikali ya ccm
ReplyDeleteBaba wa familia akishindwa kuwa na sauti basi kila mmoja anajifanyia anachotaka. Mama anaweza kurudi usiku wa manane au asubuhi yake. Watoto wakike nao wanaweza kuleta wanaume hapo nyumbuni. Wakiume nao wanaweza kuwa wafuta bangi, wezi n.k.Familia ikifikia hapo lazima patakuwa hapakaliki.Hivi wanasiasa na viongozi wetu wangazi za juu wanatupeleka wapi. Naomba JWTZ iingilie kati bora tutawaliwe na wanajeshi.
ReplyDelete