WOLPER ATUPIWA VIRAGO KWENYE JUMBA LA KUPANGA.
Posted on
May 6, 2013
|
No Comments
STAA wa filamu za Kibongo, ''Jacqueline Wolper Massawe'' anadaiwa kutupiwa nje na baadaye kuzuiliwa vyombo vyake kwenye ile nyumba ya kifahari ya kupanga aliyokuwa akiishi Mbezi Beach, Dar es salaam.
Madai hayo yalitua kwenye dawati la Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo ilielezwa kuwa ishu hiyo ilijiri maeneo hayo baada ya bishosti huyo kudaiwa kuwa alishindwa kulipa kodi ya pango ya mwezi mmoja ambayo ni Dola 1,500 (zaidi ya Sh. milioni 2.4 za madafu).
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyekuwepo eneo la tukio, Wolper aliwatuma ndugu zake kwenda kuchukua vyombo hivyo lakini walipofika mama mwenye nyumba (jina tunalo), aliwazuia na kumpigia simu staa huyo akimwambia kuwa anatakiwa kulipa fedha kabla ya kuchukua vitu vyake.
“Wolper alipopigiwa simu alikuja juu na kumwambia mama mwenye nyumba kuwa kama anamfuatilia eti atamfunga kama mume wa mama huyo alivyofungwa na kumwambia kuwa atampelekea polisi wakamkamate,” alidai mtu huyo.
Sosi huyo aliendelea kudai kuwa baada ya kuona soo limekuwa la kutishana, mama huyo alikwenda kumfuata mjumbe wa nyumba kumi aliyefahamika kwa jina moja la Musa na kumueleza kisha kumuomba asimamie zoezi hilo.
Mwandishi wetu hakuishia hapo, alimtafuta shemeji wa mama mwenye nyumba aliyetajwa kwa jina moja la Jamal ambaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kwamba suala hilo lilimalizika ambapo vyombo vya Wolper vilitolewa kwa ajili ya kufanya usafi kwani kuna mtu mwingine alikuwa akihamia.
Mjumbe wa Nyumba Kumi, Musa alipotafutwa kwenye simu yake ya kiganjani ili kuzungumzia sakata hilo alikiri kufikishiwa malalamiko ya Wolper.
Alisema kuwa msanii huyo alikuwa hajamaliza kulipa fedha, akawatuma ndugu zake wakachukue vitu vyake lakini kabla hawajavichukua mama mwenye nyumba aliwazuia mpaka alipwe chake na alipotimiza hilo ndipo akaachiwa vitu vyake.