photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > KATIKA AJIRA YAKO YA KWANZA

KATIKA AJIRA YAKO YA KWANZA

Posted on Jun 27, 2013 | No Comments


KATIKA AJIRA YAKO YA KWANZA (TIP #4/5)
Jana tulieleza tip #3 katika ajira yako ya kwanza ni kujiwekea mipaka katika kikomo cha kumaliza kazi zako ili kuzuia mwili na akili yako kuchoka. Tip ya leo ni kujituma na kuwa na ‘positive attitude’ kwa wakubwa wako wa kazi na wateja pia. Kuwa mchangamfu na mkarimu kwa wateja na kuonyesha nia ya kuwasaida wenzio katika idara yako, itakujengea heshima na kuongeza uzalishaji. Mfanyakazi bora ni yule anayejali watu na kutafuta mbinu za kutatua matatizo – huku aki ‘focus’ kwa mahitaji ya wateja na ufanisi wa kazi. Kuwahi kufika kazini dakika chache kabla ya ‘supervisor au manager’ kila siku itadhihirisha kuwa wewe ni mchapa kazi na uko tayari kufanya kazi kwa bidii. Tuma email inayohusu maswala ya kazi mapema uingiapo au kabla ya kutoka ili kuashiria kuwa upo kazini na pia kazi unazifanya. Kila wakati mhabarishe boss wako, mpe 'updates za status' za kazi au miradi unayoifanya kuonyesha mchango wako kazini. Omba msaada pale unapokwama, ila jitahidi pia kusoma na kujifunza mambo mengine kwa juhudi zako mwenyewe. Jaribu kuuliza ‘feedback’ ya utendaji wako wa kazi toka kwa supervisor wako, na ukiona unalaumiwa au kukosolewa, hupaswi kukasirika au kuweka 'beef' na mtu aliyekuripoti au kukukosoa. Unapopewa ‘constructive criticism’ ndio njia kuu pekee ya kukujenga na kujifunza. Mtu anapokueleza ukweli ujue anakupenda na anataka kukujenga hivyo unapomkasirikia unakuwa umejiharibia, ukosoajia katika ajira sio kama ya kutoka kwa wazazi au walimu wako. Tuliza munkar. Usiombe ruhusa kila mara na kukosa kwenda kazini mpaka iwe ni sababu ya msingi. Utafiti unaonyesha watu wenye tabia ya ‘abseintism’ ya kila wakati wana matatizo binafsi na waajiri huepuka kuwapa vyeo na mara nyingi watu hawa huishia kwenye orodha ya ‘redundancy’. Kila kazi utakayopewa ifanye kwa moyo na uchangamfu, pia lipatie umakini na punguza papara na haraka haraka, kumaliza kazi mapema na yenye makosa mengi haisaidii. Utapimwa upeo wako wa umakini na ustadi (positive and effective manner). Sio maujanja kukabidhi kazi kwa wakati muafaka ikiwa na makosa lukuki. Boss wako atakuona una bahatisha tu na ataanza kukufuatilia katika kazi zako kwa ukaribu sana. Jina lako la kati linatakiwa liwe ‘NINAWEZA’ na mtazamo wako uwe chanya kuli ‘support’ hilo jina la kati tena huku unatabasamu. Kesho usisahau kutembelea ukurasa wetu kupata tip #5 na ya mwisho katika ajira yako ya kwanza.Tunakutkia kila la kheri katika mafanikio yako.
 Tip ya leo ni kujituma na kuwa na ‘positive attitude’ kwa wakubwa wako wa kazi na wateja pia. Kuwa mchangamfu na mkarimu kwa wateja na kuonyesha nia ya kuwasaida wenzio katika idara yako, itakujengea heshima na kuongeza uzalishaji. Mfanyakazi bora ni yule anayejali watu na kutafuta mbinu za kutatua matatizo – huku aki ‘focus’ kwa mahitaji ya wateja na ufanisi wa kazi. Kuwahi kufika kazini dakika chache kabla ya ‘supervisor au manager’ kila siku itadhihirisha kuwa wewe ni mchapa kazi na uko tayari kufanya kazi kwa bidii. Tuma email inayohusu maswala ya kazi mapema uingiapo au kabla ya kutoka ili kuashiria kuwa upo kazini na pia kazi unazifanya. Kila wakati mhabarishe boss wako, mpe 'updates za status' za kazi au miradi unayoifanya kuonyesha mchango wako kazini. Omba msaada pale unapokwama, ila jitahidi pia kusoma na kujifunza mambo mengine kwa juhudi zako mwenyewe. Jaribu kuuliza ‘feedback’ ya utendaji wako wa kazi toka kwa supervisor wako, na ukiona unalaumiwa au kukosolewa, hupaswi kukasirika au kuweka 'beef' na mtu aliyekuripoti au kukukosoa. Unapopewa ‘constructive criticism’ ndio njia kuu pekee ya kukujenga na kujifunza. Mtu anapokueleza ukweli ujue anakupenda na anataka kukujenga hivyo unapomkasirikia unakuwa umejiharibia, ukosoajia katika ajira sio kama ya kutoka kwa wazazi au walimu wako. Tuliza munkar. Usiombe ruhusa kila mara na kukosa kwenda kazini mpaka iwe ni sababu ya msingi. Utafiti unaonyesha watu wenye tabia ya ‘abseintism’ ya kila wakati wana matatizo binafsi na waajiri huepuka kuwapa vyeo na mara nyingi watu hawa huishia kwenye orodha ya ‘redundancy’. Kila kazi utakayopewa ifanye kwa moyo na uchangamfu, pia lipatie umakini na punguza papara na haraka haraka, kumaliza kazi mapema na yenye makosa mengi haisaidii. Utapimwa upeo wako wa umakini na ustadi (positive and effective manner). Sio maujanja kukabidhi kazi kwa wakati muafaka ikiwa na makosa lukuki. Boss wako atakuona una bahatisha tu na ataanza kukufuatilia katika kazi zako kwa ukaribu sana. Jina lako la kati linatakiwa liwe ‘NINAWEZA’ na mtazamo wako uwe chanya kuli ‘support’ hilo jina la kati tena huku unatabasamu. Kesho usisahau kutembelea ukurasa wetu kupata tip #5 na ya mwisho katika ajira yako ya kwanza.Tunakutkia kila la kheri katika mafanikio yako.

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru