WASIA WA SHEKH PONDA MUDA MFUPI KABLAYA KUTEKWA NA ASKALI KANZU,MOI.
Sheikh Ponda alisema Natambua kwamba wapowanaokerwa na harakati hizi, natambua wapo wanaojali harakati hizi bila kujali imani zao iwe ndani ya serikali ama nje ya serikali.
Lakini kukwepa kusema ukweli ni kuahirisha vurugu nchini, nisiposema mimi wapo watakaosema kwa sauti kali kuliko yanguna wanaweza kuwa hatari (kama wanavyoniita) zaidi yangu tofauti na serikali inavyonitazama mimi, na hapo wajukuu zangu wataishi kwa wasiwasi zaidi
maoni yangu.
..........
Harakati zozote za kumnyamazisha shekh Ponda kudai haki za wanyonge, harakati zozote za kuwanyamazisha wanaharakati kamwe hazitokuwa suruhisho la tatizo.
Watu wenye mtizamo kama Ponda ni wengi sana Tanzania. Watu wenye ufasaha na ufahamu wa mambo zaidi ya shekh Ponda ni wengi, kumnyamazisha Ponda mmoja ni kutengeneza mamilioni ya Ponda wengine zaidi.
Naisihi serikali kuacha woga bali kuyatatua matatizo ya watanzania. Kuwapiga, kuwafunga, kuwanyanyasa watetea haki ni bure bali ni kuahirisha vuguvugu za kudai haki na siku ikifika nguvu inayotumika sasa haitosaidia.