HIVI UNAONAJE IKITOKEA COLLABO YA YOUNG KILLER, YOUNG DEE, DOGO JANJA NA M-RAP???? SOMA HAPA KISHA TUPE MAJIBU
Posted on
Jan 23, 2014
|
No Comments

Kwa tafiti ndogo tu iiyofanywa na Bongoclan inaonyesha kua mashabiki wengi wa wasanii hawa wanadhani kua hakuna urafiki mzuri kati ya wasanii hawa, kwa mfano wengi wanaamini kua kuna bifu kati ya Dogo Janja na Young Killer. Utafiti uliofanywa na website hii umegundua kua hakuna bifu kati ya wasanii hawa.
Kwani siku za hivi karibuni wameonekana maeneno mbalimbali wakila bata pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali. Swala kubwa na ambalo nahisi linaweza kuulizwa na wengi ni je katika kukutana kwao walishawahi kufikiria kufanya ngoma pamoja?? Nikimaanisha ngoma moja ambayo ndani watakuemo wote wanne yani Young Killer, Young Dee, M-Rap na Dogo Janja?
Kwa nini Bongoclan Tunaamini kama wasanii hawa kama wataamua kutoa ngoma pamoja itakua HIT TRACK! Kwanza vichwa vyote vinne vimesimama kimashairi na kila mmoja ana style yake tofauti na mwenzake jambo ambalo naamini litaleta mvuto katika wimbo huo.
Sababu ya pili ni kua itaweka attention kwa mashabiki kwani watataka kujua nani atamfunika mwenzie katika nyimbo hiyo. Ukizingatia kila mtu ana mashabiki wake so kutakua kuna kauhasama ka mashabiki wa nani wanaamini nani atafunika zaidi.
Timu nzima ya Bongoclan inapanga kukutana na wasanii hawa na kuwauliza wanalichukuliaje wazo hili na siku si nyingi tutauja na majibu ya maswali hayo. Kama una swali lolote ungependa tuwaulize unaweza tutumia katika email yetu