KUTOKA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR.
Posted on
Jun 26, 2012
|
No Comments
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Mohamed Aboud Mohamed kwa mwaka 2012/2013 katika Kikao cha Baraza hilo kinachoendela huko Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwenye baraza la Wawakilishi jana
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar DR. Khalid Salum Mohd akiongoza jopo la watendaji waandamizi wa Wizara yake kufuatilia Hotuba ya Wizara yao Iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed katika Baraza la wawakilishi Zanzibar.
