Milovan ndani ya wekundu.
Posted on
Jun 1, 2012
|
No Comments
Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic.
ILIBAKI kidogo tu Simba impoteze Kocha Mkuu, Milovan Cirkovic baada ya kuamua kutosaini mkataba mpya kutokana na kutaka mambo kadhaa yarekebishwe, kubwa likiwa ni suala la mshahara wake.
Imeelezwa Simba imekubali kumlipa mshahara wa dola 8,000 (zaidi ya Sh milioni 12) kwa mwezi na mkataba utakuwa wa mwaka mmoja ambapo Simba watalazimika kumlipa kocha huyo zaidi ya Sh milioni 153 ambazo ni mshahara wake kwa miezi 12.
Simba imekuwa ikimlipa Milovan mshahara wa dola 6,000 (zaidi ya Sh milioni 9) kwa mwezi, lakini baada ya kumaliza mkataba wake mwezi uliopita, kocha huyo raia wa Serbia alitaka uongezwe hadi dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 16), ikiwa ni pamoja na mkewe kupewa tiketi ya kwenda na kurudi atakapomtembelea mara moja kwa msimu akitokea Serbia.
Milovan aliamua kuondoka nchini bila ya kusaini mkataba mpya na Simba, hali ambayo ilizua hofu lakini habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza wamekubaliana na uongozi wa Msimbazi ofa hiyo ya dola 8,000 (zaidi ya Sh milioni 12).
Mbali na hivyo, Milovan alitaka apewe gari la kutembelea kama kocha lakini pia aishi kwenye hoteli nzuri zaidi ya hapo anapoishi. Simba haikuwa na tatizo na mengine yote yaliyobaki, isipokuwa mshahara ulionekana mkubwa sana.
Akizungumza jana kutoka kwao Serbia, Milovan alisema ana mapenzi makubwa na Simba na yupo tayari kurejea kuifundisha na si timu nyingine Tanzania.
“Tumeanza mazungumzo na Simba, najua tutakubaliana. Nataka kuendelea kuifundisha Simba kwa kuwa nina mapenzi nayo makubwa,” alisema Milovan.
Habari za kutoka ndani ya Simba zimeeleza, jana mchana Milovan alifanya mazungumzo ya simu na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na wakayaweka mambo sawa.
Kaburu alipoulizwa alikiri kuwa watamaliza suala hilo baada ya siku chache na wamekuwa wakiendelea na mchakato. “Tunaendelea kuwasiliana na kocha, tupeni muda kidogo tutawaambia kila kitu kilipofikia,” alisema Kaburu