ATIWA MBARONI KWA KUJIFANYA YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UGANDA.
Posted on
Oct 16, 2012
|
No Comments

Pichani ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mh. Sam Kutesa.
Kijeba
mmoja mwenye umri wa miaka 33 nchini Uganda ametiwa korokoroni na
polisi nchini Uganda baada ya kujifanya yeye ni Waziri wa mambo ya Nje
wa Uganda Sam Kutesa na kudai shilingi milioni 165 kwa muwekezaji mwenye
asili ya Kiasia.
Jamaa
huyo mfanyabiashara kutoka wilaya ya Wakiso mwenye umri wa miaka 33
Collins kato, ambaye pia hujulikana kwa jina la Moses Barigye amekamatwa
mjini Kololo mjini Kampala na baadae kukabidhiwa kwa mikononi mwa
polisi.
Kukamatwa
kwa bw. Kato kunafuatia malalamiko ya Vasavada Asis mmiliki wa Kampuni
ya Mara Group iliyopo Kololo, ambaye aliwataarifu maafisa usalama kuwa
Kato amekuwa akimbugudhi na kudai fedha kutoka kwake.
Inadaiwa
kuwa Bw. Kato alikuwa akimwambia muwekezaji Asis kuwa yeye kama Waziri
anahitaji fedha kwa ajili ya ziara ya kikazi nje ya nchi kwenye mkutano
wa kimataifa na kuwa atailipa kwa kumuunganishia mikataba poa ya za
serikalini.
Kwa
mujibu wa Msemaji wa Polisi wa Kampala Metropolitan Ibin Ssenkumbi,
mfanyabiashara huyo aliingia kwenye mstari na kuwataka wafanyakazi wake
kuweka fedha hizo kwenye mfuko na kumpelekea Kato.
Lakini
machale yaliwacheza baadhi ya wafanyakazi hao waliokuwa na namba ya
simu ya Mh. Waziri Kutesa na kuamua kumpigia na kumuuliza fedha hizo
tukuletee wapi? Jambo lilimshtua na kushangaa fedha na za nini tena
kutoka kwa naniii..???
Baada
ya hayo taarifa ilifikishwa polisi, ambapo sasa wao walijifanya ni
wafanyakazi wa Nara Group na kuwa wakutane wamkabidhi fedha zake, ambapo
alipotia timu aliishia kucheza na pingu na sasa anajuta kujifanya
waziri.