photo NAAZ_zpsd0bbd510copy_zps37715af5.jpg
 photo NAAZ_zpsd0bbd510.jpg
Nafasi Ya Matangazo
> > RAIS CHINA KUSAINI MKLATABA UJENZI WA BANDARI BAGAMOYO

RAIS CHINA KUSAINI MKLATABA UJENZI WA BANDARI BAGAMOYO

Posted on Mar 23, 2013 | No Comments


Rais wa China, Xi Jinping 
Dar es Salaam. Rais wa China, Xi Jinping anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara ya siku moja, ambapo pamoja na mambo mengine atasaini mikataba 17, kati ya nchi hiyo na Tanzania, ukiwamo wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Ujenzi huo utakaofanywa na Kampuni ya Merchants Holding ya China, utakwenda sambamba na ujenzi wa barabara inayounganisha bandari hiyo na Reli ya Kati na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara).

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema ujio wa rais huyo aliyechaguliwa wiki mbili zilizopita, utakuwa wa manufaa makubwa kwa Tanzania.

“Mbali na mkataba huo pia tutasaini mikataba wa kidiplomasia. Vilevile, China imefungua soko la Watanzania kuuza tumbaku nchini humo na mkataba wa kuliendeleza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),” alisema Membe.

Waziri huyo alisema kiongozi huyo wa China pia atafungua jengo la kisasa la mikutano la Mwalimu Nyerere.

“Kwa kuwa anakuja Afrika kwa mara ya kwanza huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza, Jinping pia atatoa hotuba yake juu ya msimamo wa China kwa Tanzania na Afrika kwa jumla,” alisena 

Toa Maoni Yako Kwa Uhuru