DK MWAKYEMBE ATEMBELEA UKARABATI WA MABEHEWA YA MRADI WA TRENI YA WAKAZI WA DAR !
Posted on
Jul 10, 2012
|
No Comments
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe akitambulishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kwa viongozi wa TRL na wale wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli TRAWU mara alipowasili katika Karakana ya TRL.Waziri Mwakyembe akipata maelezo ya jinsi ya ukarabati wa mabehewa 14 unavyoendelea kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu wa kwanza kulia.Baadhi ya mabehewa yanayokarabatiwa kwa ajili ya huduma ya usafiri kwa Wakazi wa jiji la Dar.Viberenge viwili malum vikijitayarisha kuondoka kuelekea Ubungo wakati wa ukaguzi wa njia ya reli ambayo itatumiwa na treni ya abiria ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam inayotarajiwa kutoa huduma hapo Oktoba mwaka huu.