Mtuhumiwa huyo almaarufu kwa jina la (Chewaja) alikuwa ni mpangaji katika nyumba ya marehemu. Ni mzaliwa wa Singida mkazi wa Arumeru mashariki. Mtuhumiwa amekamatwa Dodoma akiwa kwa mganga wa kienyeji. Chewaja awataja alioshirikiana nao katika mauaji hayo mmoja wapo ni kada wa CCM na pia ni Mwenyekiti wa Kijiji. Vilio vilitawala baada ya mtuhumiwa huyo kurudishwa kijijini chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi kuonyesha alikoficha vifaa vya mauaji, wananchi walipandwa na hasira wataka kumuua askari wakazuia. Silaha zilizokutwa shambani kwa mwenyekiti zikiwa zimefukiwa chini ni Bunduki mbili, Kisu, Panga, na Mashine ya kukatia miti iliyotumika kumchinjia marehemu. Inasemekana alifanya mauji hayo kwa ujira wa shilingi za kitanzania milioni mbili (2,000,000) na hata uko singida alikimbia kesi ya mauaji..