HUU NDIO MFUMO WA YANGA CHINI YA KOCHA MPYA..VIUNGO MSITU
Posted on
Jul 9, 2012
|
No Comments
Tom Saintfiet.
KOCHA mpya wa Yanga, Tom Saintfiet, ameweka wazi kuwa mfumo wa 4-5-1 ndiyo atakaoutumia kwenye mechi zake.
Mfumo huo ndiyo unaotumiwa na Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Milovan Cirkovic, katika upangaji wake wa kikosi cha kwanza.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Saintfiet alisema huo ndiyo mfumo anaoutumia katika upangaji wa timu kwa kuwachezesha viungo wengi.
Saintfiet alisema lengo la kujaza viungo ni kuona timu inacheza soka la kisasa ambalo anaamini ndilo litakalomwezesha kupata ushindi.
Alisema amefurahi kukuta Yanga kuna viungo wengi wenye uwezo kama Haruna Niyonzima, Juma Seif ‘Kijiko’, Nurdin Bakari, Frank Domayo na Athumani Idd ‘Chuji’.
“Mfumo ninaopenda kuutumia ni wa 4-5-1, wakati mwingine nabadilisha kulingana na aina ya wachezaji nilionao au timu ninayocheza nayo.
“Lengo kubwa la kuwajaza viungo watano na kumuacha mshambuliaji mmoja ni kutaka kuona timu inacheza soka la kisasa, tayari nimeanza kazi ya kuwafundisha vijana wangu mfumo huo,” alisema Saintfiet.