KIVUMBI CHA KAGAME CUP KUTIMKA LEO TAIFA.
Posted on
Jul 14, 2012
|
No Comments
Baada ya timu za Tusker ya Kenya na Ports ya Djibouti kuwasili jana jioni na kukamilisha idadi ya timu kumi na moja zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame yanayoanza leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi leoa ni APR ya Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini itakayoanza saa 8 kamili mchana na kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico ya Burundi.
Timu zote kutoka nje zimeshapangiwa viwanja vya mazoezi ambapo zitavitumia kwa mujibu wa ratiba ambayo imepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).