MAJAJI WOTE WA AMERICAN IDOL KUONDOKA
Posted on
Jul 14, 2012
|
No Comments
Jana Steven Tyler alithibitisha kuwa ataondoka kama jaji wa American Idol baada ya kuwepo kwa miaka miwili tu, jana hiyo hiyo, Jennifer Lopez alidokeza kuwa naye anaweza kuacha na kufanya mambo mengine.
Sasa hivi chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Us Weekly kuwa jaji mwenza na Tyler na Jlo, Randy Jackson naye ana mpango wa kuondoka kwenye panel ya majaji lakini ataendelea kuwepo kufanya kazi ya kufundisha tu kwenye show hiyo.
Tayari mwanamuziki Mariah Carey anazungumzwa kuwa anaweza kushika nafasi ya ujaji itakayoachwa wazi na Jennifer.
Majaji wengine wapya ambao wanadaiwa wanaweza kuongezwa ni pamoja na Fergie na Adam Lambert.